Matiang’i kuwachikiwa iwapo tu atatulia na kuwacha mambo ya siasa

0
6

Huenda aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani daktari Fred Matiang’i, akawa na la kutabasamia iwapo mambo yaatakwenda sambamba na ahadi walizozitoa mahasibu wake.

Duru kadhaa zimethibitisha kwamba wabunge watatu kutoka Kisii walifanya kikao na rais William Ruto katika ikulu kutafutia Matiang’i mwafaka. Wabunge hao ni Patrick Osero wa Borabu,Daniel Manduku wa Nyaribari Masaba na Anthony Kibagendi wa Kitutu Chache ambao ni kutoka chama  cha ODM.

Kwenye mkutano huo,iliafikiwa kwamba,ndiposa Matiang’i aokolewe kutoka kwa meno ya DCI,itabidi waziri huyo wa zamani,akome kilichotajwa kama sarakasi na azame na kutulia kabisa machoni pa uma.

Kisha rais Ruto kwa upande wake,ametoa ahadi ya kuangazia masaibu yake bila kuingilia shughuli za DCI.Kutokana na hayo mbunge wa Borabu Patrick Osero aliyetarajiwa kuwa mwenyeji wa Matiang’i pamoja na viongozi wengine kutoka eneo la Kisii jumamosi katika mkutano wa kuchangisha pesa katika kanisa la Mogusii SDA,amesema hatahudhuria,hatua ambayo ikawayumbisha wale ambao walitarajiwa kuwapokea kama mwenyeji

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here