Viongozi wa Azimio sasa wadai viongozi wa Kenya Kwanza wafungue sava za IEBC

0
6

Maandamano na mikutano ya mara Kwa mara kwa chama Cha Azimio si jambo geni hapa nchini . Bado
chama hiki kina Madai kuwa uchaguzi wa Agosti katika mwaka uliopita haukuwa wa haki na kura zao ziliibiwa.
Pamoja na kuwa katiba ya Kenya na Ile ya uteuzi mpya wa makamishana wa I.E.BC ilikua katika
upande wa Chama Cha Kenya kwanza Azimio iliweza vilevile kuipa serikali ya rais Ruto makataa ya siku 14 ya kuandamana iwapo sava za uchaguzi wa mwaka uliopita pamoja na kushusha gharama ya bidhaa muhimu Kwa mwananchi hazitaangaziwa.

Wakiongea katika Ibada ya kanisa la AIC kaunti ya machakos, Martha Karua pamoja na Kalonzo Musyoka walisema kuwa serikali ya rais William Ruto imeshindwa kutimiza ahadi zake Kwa wananchi
Kwa upande wake Rais Ruto ametupilia mbali matakwa ya kufunguliwa kwa sava za IEBC akisema kuwa hakuna sehemu yoyote ya katiba ya Kenya inayoruhusu au kuwapa kibali ya kufungua sava hizi
Naibu wa rais vilevile akiangazia Hali mbaya ya uchumi wa taifa ameweza kuuulaumu uongozi wa rais
mstaafu Uhuru Kenyatta ambapo alisema kuwa kulikuwepo wizi wa shilingi bilioni 16 za umma .
Alielezea kuwa shilingi bilioni Kumi na sita ziliibiwa siku mbili kabla ya uchaguzi na zingine bilioni 10 kuibiwa wakati wa ombi wa uchaguzi huo kupingwa. Gachagua alisema kiwa Hali mbaya ya uchumi umechangiwa na
wizi wa fedha hizo.
Swali lililosalia Kwa wananchi Kwa sasa ni iwapo matukio ya kutoelewana baina ya serikali ya rais Ruto
na Ile ya raila odinga yatafikia kikomo na iwapo yatafikia kikomo, je ni lini?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here