Mradi wa project 47 kusaidia hospitali kwa kusambaza madawa za kusaidia wagonjwa

0
2

Hospitali ya rufaa ya Moi,mjini Voi ni moja ya vituo vya afya viliyoko katika kaunti ya Taita Taveta na hupokea wagonjwa wengi wa dharura kila siku kutokana na magonjwa mbalimbali na pia ajali zinazotokea kwani hospitali hio ipo karibu na barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi.

Wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura kwa sasa ni wengi na idadi hio huzidi kuongezeka kila siku. Wagonjwa wanaohitaji huduma hizo ni wale waliohusika na ajali za barabarani na hivyo huhitaji msada wa haraka kwani kuchelewa kidogo huenda ikasababisha maafa zaidi…

Hali hii ya kukosa vyumba vya kutosha pamoja na vifaa muhimu vya kuwashughulikia imepelekea hitaji la ufadhili wa kuboresha huduma kwenye kituo hicho ili kupunguza vifo vya wagonjwa kutokana na kuchelewa kupokea huduma kwa wakati…

Mradi wa project 47 umeweza kunusuru hospitali hiyo kwa kufadhili shilingi zaidi ya millioni tano ili kuhakikisha kuwa vinasaidia kwa huduma za humo ndani na pia kuelimisha wafanyikazi wa vitengo vya dharura katika kituo hicho Cha afya…

Hata hivyo waziri wa afya kaunti hiyo,gifton mkaya amesema kuwa huduma za hospitali hio imeimarika pakubwa ikilinganishwa na hapo awali… 

Viongozi wa kaunti hio wamesema kuwa watashirikiana na mashirika mengine nchini ili kuhakikisha kuna huduma Bora kwa wote…

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here