Idara ya mahakama, viongozi wa kidini pamoja na washikadau katika vitengo mbalimbali wanalaumu baadhi ya wazazi kuwalazimisha wanao kwa biashara ya uuzaji wa dawa za kulevya. Aidha inasemekena kuwa baadhi Yao wanawahusisha wanao kwa biashara ya ukahaba.

Hali ya uchumi ikizidi kuwa ngumu katika pande tofauti ya nchi kila uchao,baadhi ya wazazi wengi wewageuzia wanao kujihusisha na shughuli zinazoambatana na utovu wa maadili katika jamii…
Watoto wasichana sasa wameanza kazi ya kuuza miili zao huku wavulana wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya…
Hakimu mkuu wa mahakama ya Thika,Stella Atambo anasema kuwa wao hupitia wakati mgumu wanaposhughulikia kesi kuhusiana na watoto wa umri mdogo kujihusisha na uhalifu…
Mkurugenzi wa kaunti ndogo ya Thika magharibi anaehusika na maswala ya elimu maeneo hayo Moses sifuna, ametoa onyo Kali kwa wazazi wanaotelekeza watoto wao na kutowapeleka shuleni ili kuwahusisha na biashara haramu…
Aidha viongozi Hawa wametoa sare za shule kwa wanafunzi kutoka vitongoji duni ambao ingewapelekea wao kutojiunga na shule ya upili kutokana na ukosefu wa karo na pia sare za shule…