Viongozi wa dini wasema kua umaskini ndo chanzo cha ukosefu wa uslama nchini

0
0

Viongozi wa dini na maafisa wa utafiti katika ngazi za usalama wakizia kuwa huenda umaskini na ufisadi
ndio vyanzo vya ukosefu wa Usalama Nchini . Wakuu hao wamesema Hali ya Maisha imefanya vijana
wengi walioacha shule kuwa rahisi kumulikwa na wanamgambo wa Al-shabaab ili kuwasaidia katika
Utendakazi na utekelezaji wa mashabmbulizi haswa Maeneo ya Garissa.
Ufisadi na Umaskini sababu za kudorora kwa usalama
Hamasisho la Viongozi wa dini kumaliza Ugaidi

Hali ya usalama ikiendelea kuwa kero,bukudha na kuwakata maini wanachi na serikali Viongozi wa
dini wakiongozwa na Sheikh Ibrahim Lethome wamejitokeza kusema umaskini na ufisadi katika
vitengo vingi humu Nchini ikiwemo vitengo vya usalama ndio imechangia pakubwa kusorota kwa Hali
ya usalama,
Pamoja na hayo mtafiti wa maswala ya usalama Usama Hassan ameongezea kuwa Wanamgambo wa
Al-shabaab wametumia nafasi hiyo ya umaskini na ufisadi kupenya katika vitengo za usalama wa
humu Nchini na pia kuwarai vijana kujiunga nao na kuwasaidia kutekeleza mashambulizi huku
wakilipwa mapeni makubwa ili kufukuza umaskini uliowakapa koo.
Hata hivyo kamati ya usalama eneo la Garissa yakutana na viongozi wa dini kutafuta mbinu za
kukomesha Ugaidi , kamishena wa eneo la kaskazini Mashariki John Otieno amewataka viongozi wa
kidini kutumia ushawishi wao katika jamii kutambua na kurekebisha mienendo isiyofaa.. Viongozi
hao wa kidiniw walikubali kushirikiana na serikali kuwaelekeza waumini makanisani na misikitini

Romeo Were Mtazamo wa Dira ya Tandao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here