Kenya imejumuika na Mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku ya viti au baiskeli za
magurudumu yaani wheelchair duniani. sherehe hii imefanyika katika kituo Cha walemavu cha
bombolulu kaunti ya Mombasa.
Maadhimisho haya yanalenga kuhamasisha watu kuhusiana n umuhimuwa viti hivi vya magurudumu katika maisha ya watu wanaishi na ulemavu. Baadhi ya matukioyaliyofanyika Leo hii katika kituo hiki Cha walemavu ni pamoja na matembezi na maandamano ya amani.
Kulinganana na mwenyekiti wa kitu Cha walemavu Cha bombolulu, Peter Ouma, siku hii
inasherehekewa Kwa kuwa ni siku muhimu sana kwani zimewasaidia walemavu katika kutembea na
kufanya shughuli zingine kama watu wa kawaida.
Shirika la apdk vilevile liliweza kuhudhuria maadhimisho haya na kuelezea kuwa shirika hili limekua
katika mstari wa mbele katika kuwatafuta na vilevile kuwafanyia uchunguzi ili kubaini haswaa ni aina
gani ya viti hivi wanahitaji .

Wameweza pia kushirikiana na mashirika mengine kama vile national fund for the disabled of kenya na wahisani wengi ili kupeana viti licha ya hitaji lake kuwa kubwa sana Aidha walemavu waliweza kuhamasishwa kuwa ulemavu ni Hali ya kawaida na ni jukumu la jamii kuwapa nafasi sawa na wengikwani Wana uwezo
Aidha ,mwakilishi wa eneo hili alielezea kutengwa Kwa walemavu katika jamii na aliangazia juhudi za
serikali katika kuweka maeneo mbalimbali kama vile hospitali na benki vifaa vitakavyo rahisisha
shughuli za watu wanaishi na ulemavu.