Maradhi ya ngozi yanaendelea kutatiza jamii ndogo ya ilimayang inayoishi fuoni mwa ziwa Turkana katika Kijiji Cha Kapua. Maumbile Yao yamewafanya kukosa kuwa na matundu ya kupumua Wala kutoa jasho mwilini na hivyo wengi wao wamekua wakifariki huku wachache waliosalia wakilazimika kubeba maji Ili wajimwagie Kila wakati.

Katika mji wa lodwar kaunti ya turkana,Mzee mmoja mkaazi wa kalokotung ambaye ni miongoni mwa watu kutoka jamii ya lamayang ambao wako na ulemavu wa ngozi .Ngozi yake Haina matundu ya kutoa jasho na hivyo lazima ajimwagie maji Ili kutuliza joto mwilini mwake.
Watu Hawa ambao idadi Yao kufikia Sasa inakisiwa kuwa mia moja tu nchini kote,wamezaana na kulingana na uzao wao,watoto waliozaliwa pia wanapatikana kuwa na jini kama za wazazi wao.Wavulana wanakosa kumea nywele kichwani na sura zao huwa na umbo la Yai na ngozi Yao huonekana kuwa na magamba kama ya samaki
Baadhi ya watoto hao ni pamoja na kaka abel mwenye umri wa miaka kumi na miwili ambaye anasoma katika shule ya msingi ya erait academy katika kaunti ya lodwar.Mtoto huyo na kaka yake wanalazimika kustahimili hali ngumu ya joto shuleni kutokana na hali Yao wakiwa na ari ya kutafuta masomo
Huku hali ya ukame na kiangazi ikiendelea kukumba kaunti nyingi kote nchini,Kwa jamii hiyo ya ilimayang wanaendelea kuathirika zaidi kutokana na maumbile Yao.Ukosefu wa fursa ya ngozi Yao kupumua inafanya nyuzi joto Yao kuwa juu kiwango kwamba ambacho wakiwa wagonjwa madaktari wanashindwa kutambua kinachowasibu