Mbunge Peter Kaluma akataanwa na hatua ya serikali kuihalalisha LGBTQ

0
3
Pride flag. HBTQ flag. Rainbow flag. Fluttering in the wind

Baada ya kifo Cha mwanaharakati Edwin Chiloba aliyepatikana amefariki mwezi mmoja uliopita,wapenzi
wa jinsia moja wamekuwa katika harakati ya kuhakikisha kuwa haki zao zimeangaziwa na serikali pamoja
na mahakama kuu.

Ombi lao la muda mrefu hatimaye limejibiwa kwani mahakama ya juu kuamua kuwa wana haki ya kujiandikisha na kuwa wanachama wa muungano wa kijamii.
Swala hili la iwapo mashoga na wasagaji Wana haki na uhuru wa kuendeleza Imani zao,limeishi kuwa
mjadala kwa umma kwa muda mrefu.

Kufuatia kesi ilikuwa mahakamani na sasa imefikia mahakama ya juu,jumuiya hio imepata ushindi baada ya kuamuliwa kuwa bodi ya usajili wa vyama visivyo vya kiserikali wanapaswa kuwaruhusu mashoga na wasagaji kusajiliwa.
Aidha mbunge wa homabay peter kaluma ansema kuwa atarejea kwa mahakama hio ili kupata chanzo
Cha kufanya uamuzi kama huo. (Ups)
Mbunge huyo pia anasema kuwa,atatunga sheria itakayojumuisha sheria zote za jumuiya ya LGBTQ na
vitendo vyake. Pendekezo Hilo litawasilishwa bungeni ili kuwapa adhabu Kali kwa wale watakaokiuka
sheria za nchi.
Kaluma anasema kuwa,kuna Hana kubwa ya kifungo kisichokuwa chini ya miaka thelathini au hata kile
cha Maisha akidai kuwa vitendo vya ushoga havina utofaiti wowote na makosa mengine ya jinai kama
vile ubakaji.

From Sharon Wafula a fellow reporter and Journalist at Tandao Tv Kenya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here