Viongozi wa kidini wamejitokeza kulalamikia kuhusu gharama ya juu ya Maisha ambayo huenda ikaathiri mfungo wa Ramadhan.
Maimamu kutoka bonde la ufa wameirai serikali kushusha bei ya tende ambayo ni kiungo muhimu wakati wa mfungo wa Ramadhan.
Hali ngumu ya maisha imeendelea kushuhudiwa Nchini huku Hali ya uchumi ikiwakeketa maini wakenya wengi.

Mashirika mbalimbali yakijitokeza kuishutumu serikali ya Kenya kwanza. Huku mrengo wa Azimio ambao imeipa serikali wiki mbili ili kupunguza bei ya bidhaa muhimu Nchini pasipo kusita la si hivo wataandaa maandamano kote Nchini.
Ni juzi tu tulimwona mwanasarakasi wa Sanaa Eric Omondi akiandaa maandamano Hadi bunge huku akilalamikia Hali ngumu ya Maisha
Hivi Sasa maimamu kutoka bonde la ufa wameirai serikali kushusha bei ya tende kwa kutoa Ushuru ndiposa gharama hii ya juu isiathiri mufungu wa mwezi mtakatifu wa Ramadhan.
Kwa mjibu wa maimamu hao Hali ya uchumi imekuwa ngumu zaidi na tende ni kiungo muhimu haswa wakati wa mfungo huu wa Ramadhan .
Maimamu hao hawakukosa kuongelea swala la Mapenzi ya jinsia moja kwa kulikashifu vikali ambapo
koti iliamuru itakuwa halali hapo jana