Jee!! Bwana Odinga alifanya ujasiri kupipinga serikali ya Ruto?

0
4

Kinara wa upinzani Bwana Raila Odinga alitoa kauli zenye msisitizo na matokeo yenye madhara makubwa. “tuko tayari kufa tukipigana kwa haki” haya ni maneno yake kinara huyo.

Muungano wa Azimio umepigwa na mawimbi si haba hasa baada ya kauli yake kiongozi huyu anayedai ana haki kikatiba kupuzilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka uliopita.

Usaliti wa wabunge wa chama cha Odm,matamshi ya jubilee kujiondoa kwenye muungano huo,kesi anazozikabili wakili wake danstan omari pamoja na kusimamishwa kwake kazi katika umoja wa afrika ni baadhi ya changamoto sugu zinazomkabili kiongozi huyu.

Odinga alipotangaza kutoitambua serikali ya Bw.Ruto ndipo alilichimba kaburi lake mwenyewe kwani hakuelewa msingi wa kazi yake.

Ama kweli ni kisa cha abunwasi kukikata kiunga cha mti alichokikalia mwenyewe? Hapa kweli ni kinaya mtazamaji. Kulingana na katiba ya umoja wa mataifa hakuna kiongozi yeyote anayepaswa kuwa mbele katika kuipinga serikali,wala hakuna kiongozi yeyote anayepaswa kuhusika katika siasa za mara kwa mara.

Mnamo mwaka wa 2018 raisi mstaafu uhuru kenyatta alipendekeza kuchaguliwa kwa Raila Odinga kama mwakilishi katika umoja wa mataifa si kikazi ila kuzima debe lake. Inaakisiwa kwamba kwa kuwa mwakilishi mkuu wa umoja wa Afrika anapaswa kudumu kwa baraka za rais wa nchi yake tena kwa kumweshimu na kueneza mjadala wa amani,basi raisi mstaafu Uhuru Kenyatta alijua fika kwamba Odinga hangeshinda katika kura za uraisi mwaka uliopita,ila kwa hili ajukumike na kuleta amani kama au inavyotaka.

Raila odinga ameonekana kutotishika kabisa licha ya vitisho kutoka serikali ya kenya kwanza. Ingawa odinga alikiri kujiuzulu mwenyewe ,duru zinasema kwamba odinga kapigwa kalamu kwa kosa la kutoitambua serikali yake.

Ni kweli kusema kwamba raisi mstaafu Uhuru Kenyatta alitumia msemo wa mtumie mwizi kumshika mwizi ila mtego huu umefeli. Baada ya tume ya au kumbandua Odinga,raisi ameongeza kuni zaidi kwa kupinga safari zake Odinga katika nchi za kigeni.

Zikiwa zimesalia siku kumi pekee sasa wakenya hawajui kitakachotokea kwani mbwa sasa hayupo kifungoni. Ni vyema kwa wakenya kujihusisha na dua wasije wakayafufua maafa ya yaliolisibu taifa 2007

Jee Bwana Raila Odinga alifanya ujasiri kuupinga waziwazi hatua na Serikali ya bwana Ruto??

Zungumza nasi kwenye kurasa zetu za mtandao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here