Kundi La vijana kaunti ya Nandi laamzisha mikakati ya kukabiliana na mihadarati

0
2

Kundi la vijana Katika kaunti ya Nandi limeanzisha mpango wa kutoa hamasisho Kwa jamii dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na pombe. Hii ni kufuatia ongezeko la vijana kuangamia kutokana na unywaji wa pombe na utumizi wa dawa za kulevya.

Kundi la vijana katika kaunti ya nandi linalojumuisha waraibu walioasi unywaji pombe,viongozi na vijana  wanatumia Kila fursa kama vile mitandao ya kijamii  usanii na hata mikutano mbalimbali  kueleza madhara ya pombe miongoni mwao vijana.

Vijana hao waliamua kujumika pamoja Kwa kua vijana wengi waliosoma wanajihusisha na mihadarati  lakini wanaishia kufanya mambo yasiyokubalika na jamii Kwa sababu ya mihadarati haswa pombe haramu.

Aidha,muungano wa wanawake katika kaunti ya mombasa inataka serikali kushughulikia kikamilifu na kuttafuta suluhu ya utumizi wa mihadarati.Wanawake hao wameghadhabishwa na utumizi wa mihadarati inayochangia pakubwa uhalifu na utoovu wa usalama .Wanawake hao wasema kuwa ukosefu wa kazi miongoni mwao vijana ni sababu kuu inayowapelekea kutumia mihadarati.

Wanawake hao Sasa waiomba serikali kuu na serikali ya kaunti kuwapa vijana kazi haswa kazi za serikali Ili kuepukana na tatizo Hilo la utoovu wa usalama Kwa sababu ya mihadarati.

Serikali kuu Sasa yaombwa kuwasaidia vijana waliosoma na mwishowe kukosa kazi Kwa kuwa idadi ya vijana wanaojiunga na mihadarati na kisha kufanya mambo yasiyofaa imepanda Kwa asilimia arobaini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here