Wananchi waungana na serikali kuumaliza uhalifu Nchini

0
2

Huku serikali ya Rais William Ruto ikiendelea kuandaa magongamano na mataifa ya Afrika mashariki
kuhusu vita dhidi ya Ugaidi ambao umeshamiri na kukita mizizi kote ulimwenguni.

Serikali ya Kenya imejitia jitihada kuhusiana na kulinda mipaka na maeneo yaliyosifika kuwa makao ya wanamgambo wa Al-shabaab.


Wananchi kutoka Kaunti ya Garissa ikiwa pamoja na wazee wameghadhabika na vitendo hivi za Ugaidi
na kuapa kushirikiana na serikali ili kupambana na Tishio hili baada ya tishio ya Ugaidi kutangazwa na
mataifa ya Magharibi.
Visa za Ugaidi vimeshamiri hivi kutoka desemba mwaka Jana Hadi Sasa hivi visa saba za mashabmbulizi
vimeripotiwa eneo bunge la Fafi hasa maeneo ya Barbara mpya ya lapset inayotoka lamu Hadi nchi jirani
ya Sudan kuzini.

Japo maafisa wa polisi walifanikiwa kushika baadhi ya vigogo wa Al-shabaab katika
maeneo hayo.
Wakuu wa usalama kaunti ya Garissa wakiongozwa na commissioner wa kaunti hiyo Bossy Cherotich
walifanya kikao maalum na wazeekuafiki ushirikianao Kati ya wenyeji na maafisa wa polisi kumaliza
ugaidi. Waakazi wamelaumiwa kuwakubali magaidi Kuweka makao huko.

Hata hivyo wakazi wameahidi kusaidia kumaliza wanamgambo hao kwa vile baadhi ya shule na hospitali zimeathirika kutokana na Hali hii japo wazazi wameambiwa warejeahe watoto shuleni kwa vile mikakati imara itawekwa

Serikali ya Kenya imejitia jitihada kuhusiana na kulinda mipaka na maeneo yaliyosifika kuwa makao ya wanamgambo wa Al-shabaab.

Read more


Ubalozi wa uingereza na marekani ulitoa tahadhari kuhusiana na Tishio la ugaidi maeneo kadhaa Nchini
kama vile kaunti za Nairobi, Garissa,lamu , tana river na mandera, wananchi wote inafaa wafahamu
kuwa Cha mwenzako kikinyolewa chako tia maji ,

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here