Ziwa Ol-bolossat katika mlima Kenya Kukauka

0
8

ZIWA ol bolossat katika kaunti ya nyandarua ni ZIWA pekee la kiasili katika maeneo ya mlima Kenya na
Kwa sasa laendelea kusababisha vilio Kwa wakaazi wa eneo hili.

Lake Ol-Bolossat

Hii ni baada ya sehemu kubwa ya ZIWA hili kukauka kutokana na kiangazi kinachoendelea kushuhudiwa nchini pamoja na shughuli za kibinadamu zinazotekelezwa eneo hili .

Wakaazi wanasema kuwa ni asilimia 10 pekee ya maji ambayo imewezakusalia.
ZIWA hili linajivunia kuwepo Kwa wanyama mbalimbali kama vile viboko na ndege wa Kila aina ambao
wamewavutia watalii tangu kitambo.

Kwa sasa binaramu,mifugo pamoja na ndege wanaolitegemea ziwa hili wanaendelea kupitia wakati mgumu baadhi ya mifugo pia wakiripotiwa kuangamia.
Wakaazi wa eneo hili wanasema kuwa wanamehuzunishwa na kukauka Kwa ZIWA hili ambalo limekua
tegemeo Kwa wengi.
Wakiongozwa na mbunge wa nyandarua Faith Gitau, wanahofia usalama wao kutokana na kuwepo
Kwa wafugaji wengi wasiotoka eneo hili wakija kuwalisha mifugo yao hapa. Vilevile wanahofia
uwezekano wa shamba hili kunyakuliwa iwapo ZIWA hili litakauka kabisa
Wanaiomba serikali haswa wizara ya maji kuingilia kati ili kutoa uchafu ulioko ziwani humu ili mvua ijapo
waweze kupata maji

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here