Maisha ya Wafungwa Nchini, jee ni yepi wanayopitia

0
4

Wakati mwingi wafungwa hujikuta katika hali tatanishi wakati ambapo wao huhukumiwa jela. Huku
wengine kuhukumiwa hata kwa kukosa kujua ni kosa au makosa yapi yamewapelekea kufungwa.

Pia kuna wale wanaotiwa mbaroni kwa makosa madogo madogo kama vile kujisaidia kando ya barabara.
Tunakutana na kijana mmoja kwa jina Kevin omondibaliye gerezani kwa mashtaka kama hayo.

Wengine pia wanahukumiwa kifungo cha maisha kwa madai ya makosa kama vile ubakaji,wizi na
mengine mengi. Wafungwa hawa wanaelezea dhiki inayowapata wakiwa gerezani kwani hawana jamaa
wa karibu kutoka familia zao ili kuwafariji.

Pia wanalalamikia kurundika kwa wafungwa wengine,chakulakisicho cha afya,malazi na pahali pa kulala pia ni shida,ukosefu was maji safi ya kunywa,magonjwa yakuambukizana miongoni mwa mengine.

Serikali Ina jukumu la kuwashighulikia wafungwa hawa na shidawanazopatwa nazo Kando na hayo,rumande pia husaidia kukuza talanta za vijana wengi na pia kujihusisha na miradi tofauti
inayoleta mapato kama vile upanzi wa mboga na kupata zaidi ya 20000 kutokana na mauzo hayo.

Nixonmmoja wa wafungwa na pia anayejihusisha na upanzi gerezani humo anaelezea miradi aliyo nayo
ikiwemo,ndizi,vitunguu na karoti inayoonyesha kuwa amebadilika. Mafunzo hayo itawasaidia katika
maisha yao ya baadae.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here