Mama na binti yao wachomwa hadi kufa kwa tuhuma za mauaji

0
4

Hali ya huzuni ilitanda katika kijiji cha Magina Lari, kaunti ya Kiambu baada ya mama mmoja na bintiye kuteketezwa hadi kufa alfajiri ya kuamkia leo.

Esther Njeri, mwenye umri wa miaka 54 na mama wa watoto wanne na bintiye Lucy Wanjiru mwenye umri wa miaka 14 walikuwa wakiishi pamoja mkasa ulipotokea.

Majirani ambao walikuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio wanasema mlango ulikuwa umefungwa kutoka nje na hivyo kushuku kuwepo kwa matukio ya vifo viwili. Juhudi za kupambana na moto huo mkubwa ziliambulia patupu.

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa eneo hilo, Isaac Muchiri, anasema maafisa wa polisi wa uchunguzi wanachunguza chanzo cha moto huo.

Wakaazi wa eneo hilo wanaiomba serikali ya kaunti ya Kiambu kusambaza eneo hilo angalau kituo kimoja cha zima moto ili kukabiliana na visa vya moto katika siku zijazo.

Miili ya walioaga dunia ilikimbizwa katika hifadhi ya maiti ya Naivasha ikisubiri uchunguzi wa maiti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here