Ronaldo: nyota ambaye hakuna anayemtaka’

0
10

Cristiano Ronaldo alifanywa nyota ambaye hakuna mtu anayemtaka baada ya Ureno kuamua kuwa wanaweza kufanya vyema bila utegemezi wake.

Na hilo lilidhihirika wakati timu ya taifa ya Ureno ilipozawadia ujasiri wa kocha Fernando Santos kwa kumuacha nje nyota huyo katika kikosi cha kwanza ,kupata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Uswizi.

Ureno sasa atachuana na Morocco katika kipute cha robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.

Umekuwa wakati mgumu kwa Ronaldo, 37, mwenye umri wa miaka 37, baada ya maisha yake ya soka ya Manchester United kuisha katika hali mbaya alipotoa shutuma za hadharani dhidi ya klabu hiyo.

Ureno nayo imefanya jambo ambalo  awali halikutarajiwa- katika mechi kama 31 zilizopita na kabla ya Euro 2008 – na hatimae kumtoa kwenye kikosi chao cha kuanzia kwenye mashindano makubwa.

Bila shaka uamuzi huo haukuwa wa kijasiri tu katika michuano ya Kombe hili la Dunia  bali pia ulikuwa mkubwa zaidi kwa muda wa miaka minane wa Santos kuongoza Ureno.

Santos, licha ya kuweka kibindoni ushindi wa Euro 2016, atakuwa ametathmini hatari ya kufanyia kikosi chake mabadiliko hayo makubwa.

Iwapo Ureno wangepoteza, ni yeye angelaumiwa kwa kuchangia kuondolewa kwa timu hiyo kwenye Kombe la Dunia na sio Cristiano Ronaldo.

Badala yake, Santos alifuatilia mchuano huo kwa ukali wake wa kawaida huku Ureno ikionekana kuwa na timu iliyochangamka zaidi na kufanya mashambulizi bila ya uwepo wa Ronaldo uwanjani.

Ureno walipenya safu ya kati bila pingamizi huku Bernardo Silva na Bruno Fernandes wakitawala safu zao, na huko mbele mshambuliaji wa Benfica Ramos, 21, ambaye hapo awali alikuwa hajulikani kwa aina hii ya ufungaji, alifanya jukumu lake kwa ustadi kama mbadala wa Ronaldo.

Joao Felix ana talanta lakini uwezo wake haukuwahi kujionyesha kama ilivyokuwa usiku wa jana katika mechi dhidi ya Uswizi kwani alionekana kuwa huru, sawa na wachezai wengine wa Ureno.

Ramos alifunga Hat-trick kwa mitindo tifauti.

Ronaldo, kabla ya mchezo huu, alikuwa amecheza dakika 514 za soka la mtoano la Kombe la Dunia bila bao. Ramos alikuwa na matatu ndani ya dakika 67.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here