Machafuko na ghasia zilizuka katika bunge kuu la Senegal siku ya Alhamisi, hii ni baada ya mbunge mwanamume kumpiga mwenzake wa kike kichwani wakati wa kikao cha bunge tukio ambalo lilionyeswa moja kwa moja kwenye televisheni kuu nchini humo.

Ilikua imehitimu wakati wa uwasilishaji wa bajeti, na Amy Ndiaye Gniby alipata kutamka maneno amabayo yalimkasirisha na kupelekea mbunge wa upinzani Massata Samb kuondoka jukwaani na kuelekea kwa Amy Ndiaye Gniby wa muungano tawala wa Benno Bokk Yakaar na kumpiga.
Katikahali ya mshike mshike , Bi Gniby alimrushia kiti Bw Samb, kabla ya wabunge wengine kuingilia kati, hata hivyo machafuko hayo hayakukoma huku wabunge hao wakibadilishana mapigo na kusababisha kusitishwa kwa kikao hicho.