ROBOTI YA ASILI YA KIAFRIKA YAZINDULIWA NIGERIA

0
4

Kundi la Makampuni ya Uniccon limesema kua linatazamia kuzindua roboti ya kwanza barani Afrika yenye sura ya binadamu yenye asili ya kiafrika inayoitwa na ‘Omeife’, nchini Nigeria.

Mkurugenzi Mtendaji wa kikundi hicho, Bw. Chuks Ekwueme, ambaye alitangaza hayo katika taarifa yake jana mjini Abuja, alisema hafla hiyo itafanyika katika siku ya ijumaa.

Ekwueme alisema roboti huyo wa kike wa Kiafrika mwenye urefu wa futi sita anazungumza lugha kama huduma kwa biashara zinazohitaji kuunganisha watazamaji asilia wa Kiafrika, akiongeza kuwa ni roboti ya kazi nyingi na msaada.

Roboti hiyo inazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, na pia lugha ya kiswahili,Kiafrika, kama vile, Pidgin, Wazobia, Afrikaans na Igbo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here