Watu wawili wanaswa na karatasi za mtihani KCSE

0
3

Watu wawili kaunti ya Busia sasa wanazuiliwa na idara ya usalama ya kaunti hiyo baada ya kupatikana na karatasi za maelezo ya mitihani ya KCSE katika somo la Biolojia, Fisikia na Kemia ya mwaka huu eneo bunge la Matayos. wawili hawa na wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Busia wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Wanafunzi wa kidato cha nne wanapozidi kujiandaa katika kuukalia mtihani wao wa mwisho wa KCSE. walimu na wazazi wanaamini kuwa mtihani huo utafanyika kwa njia halali na bora na kumtunuku kila mwanafunzi tunu yake atakayovuna ndani ya miaka minne katika shule ya upili baada ya mitihani yao kusahihishwa.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza kuwa mitihani ya mwaka huu imewekewa ulinzi wa kutosha na hakutashuhudiwa kuwepo kwa wizi wa mitihani hiyo. kinyume na taarifa za wawikli walionaswana na karatasi za maelezo ya mitihani ya KCSE ya mwaka huu.  

Idara ya usalama mjini Busia inawazuilia watu wawili ambao walipatikana na karatasi za maelezo ya mitihani ya KCSE  eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia.  

Kaimu kamishna wa Busia Kipchumba Rutto amesema kuwa wawili hao walipatikana na maelezo ya mtihani wa masomo ya kemia fisikia na bayolojia ya mwaka huu na wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Busia wakisubiri kufikishwa mahakamani.

“Kuna tukio lililofanyika huko Rangwe ambako mtoto mwenye umri wa miaka kumi alinajisiwa na baadae kuuliwa. inasemekana kuwa huyu kijana ambaye ni kasisi katika kanisa la Legion Maria ndiye alitekeleza hiki kitendo huko rangwe kisha akakimbia mafichoni sehemu ya Migori kwa kanisa la Legio Maria iliyoko Kwoyo. Tulipopata taarifa hizi tulituma askari na wamemkamata. watamrudisha katika kituo cha polisi huko Rangwe na kushtakiwa kwa tuhuma ukatili huu alioufanya.” Kipchumba Ruto-Kaimu Kamishnawa Busia.
Na Juliet wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here