Mwanafarao amkung’uta Mbelgiji katika mechi ya kirafiki

0
6

Ubelgiji ilifungwa 2-1 na Misri katika mchezo wa kirafiki kabla ya kombe la dunia kung’oa nanga rasmi.
Kosa la Kevin De Bruyne na pasi ya Mohamed Salah iliihakikishia Misri ushindi licha ya wao kukosa kufuzu katika michuano ya kombe la dunia mwezi Machi.
Mostafa Mohamed aliifungia Misri bao la ufunguzi panapo dakika ya 33 baada ya De Bruyne kupoteza mpira nje  ya eneo lake la hatari na kuwapa Misri uongozi wa 1-0  kabla ya mapumziko.
Pasi maridadi kutoka kwa mshambulizi wa Liverpool Mohammed kwa mchezaji Trezeguet aliyefunga kwa mguu wake wa kushoto iliihakikishia Misri ushindi huo wa mabao 2-0.
Lois Openda aliifungia Ubelgiji bao la kufutia machozi kwenye dakika ya 76′ .

MATOKEO YA MECHI ZINGINE ZA KIRAFIKI
BAHRAIN 1-5 SERBIA
CAMEROON 1-1 PANAMA

Ikumbukwe kuwa kombe la dunia litang’oa nanga rasmi huku wenyeji Qatar wakiialika Equador ugani al-Bayt huku maandalizi wa mwishomwisho yakishika kasi.

Na Brian Simiyu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here