
Waendesha bodaboda wakihusishwa na visa vya utovu wa usalama katika maeneo mbalimbali nchini Kenya, baadhi yao katika eneo la Kivumbini jijini Nakuru wameamua kuvalia njuga mchakato wa kusafisha jina lao kwa kushirikiana na polisi katika kudumisha usalama mitaa yao.
Eneo hili la Kivumbini limekuwa kero kubwa kwa wakaazi kwa kuaminika kama sehemu ya wahalifu sugu. kutokana na sifa hasi zinazomiminiwa Kivumbini,  ingizingatiwa visa vya watu kujeruhiwa kwa visu, sasa wakaazi na wanabodaboda  katika maeneo haya waliamua kushirikiana katika kukomesha uhalifu.
“Tulikaa chini tukaona vijana wanatumaliza na tukaamua kwenda kama jamii moja ya wananyumba kumi tukatowa vijana na pia tunashirikiana na polisi kwenye mchakato wa kutafuta na kukomesha wahalifu,” Evans imbali – mwenyekiti wa Kivumbini Boda Boda
Kisa cha hivi punde cha wakaazi wenye hamaki kuchukuwa sheria mkononi mwao na kumkabili mshukiwa mmoja wa uhalifu kwa jina steve aliyeshambuliwa kitutu kwenye harakati za kuvunja duka moja la kibiashara jumamosi iliyopita.
“Anajigamba kuwa watamfanya nini, lakini nashukuru wananchi wenyewe walimshukulikia na hilo lilikuwa jambo la heri sana,” Peter Mwanzo -kamanda wa polisi -Nakuru
Mshukiwa huyu aliyeokolewa na polisi sasa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Nakuru, huku wakaazi wakitoa onyo kali kwa wahalifu ambao wanazidi kutekeleza maovu yao kuwa wembe ni ule ule.
Ukosefu wa kazi umetajwa kama sababu moja wapo ya vijana kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya na baadaye kuwa wahalifu. Ushirikiano huu wa wakaazi wa kivumbini kuamua kupiga marufuku maovu ni mojawapo wa hatua muhimu za kuigwa katika maeneo mbalimbali nchini ili kuthibiti visa vya utovu wa usalama.
Na Juliet Wekesa