Huku kongamano la mabadiliko ya tabianchi likiingia kipindi cha lala salama, macho yote yanaelekezewa kwa wawakilishi wa bara Afrika katika mazungumzo hayo. Kilele cha kongamano hilo ni taarifa ya mwisho ambayo itatolewa baada ya makubaliano miongoni mwa mataifa yote mia moja tisini na saba ya wanachama wa umoja wa mataifa.

Jambo ambalo si rahisi haswa kwa wawakilishi wa mataifa tofauti. Je, yapi haswa majukumu ya waakilishi hao kwenye mazungumzo?

Mazungumuzo na majadiliano ambayo hufanyika ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kawaida huendeshwa na wawakilishi kutoka mataifa tofauti. Wiki ya kwanza ya kongamano hilo hushuhudia wakilishi hawa wakiweka juhudi katika kuwasilisha maswala muhimu na kuwakilisha mataifa yaliyowatuma hapo.

Kila taifa huandaa mkutano kabla ya kuwatuma wawakilishi wao katika kongamano hilo .

Mwaka huu wawakilishi kutoka bara ya Afrika kwa kauli moja walitaka sana swala la ufadhili kwa mataifa na waathirika wa mabadiliko ya tabia ya nchi kuangaziwa.

Walifaulu pia kuweka swala hilo la malipo ya hasara na uharibifu kwenye ajenda ya mazungumzo lakini maswala ya utekelezaji wake yalisukumwa hadi mwaka wa elfu mbili ishirini na nne

Mohammed Adoo wa Shirika la Power Shift Afrika alisema kuwa ufadhili huo unapaswa kushughulikiwa kwa kina ili kusaidia mataifa yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na ni mujibu wa mataifa yaliyostawi kutoa ufadhili huo.

Kuhairishwa kwa mazungumzo ya ufadhili kulikuwa pigo kubwa kwa wakilishi wa bara la afrika.

Cecilia Kinuthia Njenga ambaye ni mkurugenzi wa shirika la umoja la mataifa linaloandaa kongamano hili alitaka mtaifa yanayo stawi kusaidia kukuza mataifa madogo na yayokuwa.

Kongamano la aina hii kwa kawaida hufwata mfumo wa kongamano za COP zilizotangulia na iwapo swala lolote halijazungumziwa na wawakilishi kutoka mataifa mia moja tisini na saba linasukumwa katika kongamano lijalo.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here