Chama cha UDA kinakumbwa na mawimbi kufuatia mbinu ambayo itatumika kuchagua wabunge wateule kwa ajili ya viti vya ubunge afrika mashariki (EALA). Haya yanajiri baada ya mazungumzo kati ya rais William Ruto  na wabunge kutoka mrengo wa Kenya Kwanza katika kikao ambacho kiliandaliwa katika ikulu Nairobi.

Utata umeonekana kutokea katika chama cha rais UDA kufuatia viti vya ubunge vya afrika mashariki, eala katika mbinu ambayo inapaniwa kutumika kuwateuwa watakao chukua nafsi katika bunge hili.

Usimamizi wa chama cha UDA umegawanya wanaomezea viti hivyo katika makundi matano, maamuzi haya huenda yakasabisha ufa katika uda kwani baadhi ya wanachama wanapinga hatua hii wakilalamikia kusalitiwa katika mchakato wa uteuzi ambao rais william ruto alimpa mwakilishi wa wengi katika bunge la kitaifa na seneti.

Katika mchakato unaotumiwa na uda baadhi ya wanachama wanadai kuwa unapendelea baadhi ya viongozi ukiwapa nafasi kubwa ya kuteliwa.

Uda iliwasilisha orodha ya majina ya kumi na tano kuwania viti vya ubunge wa eala waiwemo, aliyekuwa seneta wa mombasa hassan omar aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha rais cha URP kilichofutiliwa mbali Fred Muteti na aliyekuwa mbunge mteule David Sangok.

Kenya imetengewa nafasi tisa za wabunge watakao wakilisha katika bunge la eala  ambapo mrengo wa kenyakwanza ambayo ni upande wa wengi itashirikisha wagombea kumi na watano huku upande wa wachache wa Azimio ukiwa na kumi na wawili

Kenya Kwanza imetengewa nafasi tano za wabunge huku ziliosalia nne kutengewa mrengo wa azimio la umoja unaoongozwa na Raila Odinga akiwemo mwanawe Raila , Winnie Odinga na mwanawe Kalonzo Musyoka.

Uchaguzi wa kugombea nyadhifa za ubunge wa EALA utafanyika  tarehe kumi na saba Novemba wiki chache tu kabla ya atamu ya bunge la kisasa la eala mwezi ujao tarehe kumi na saba.

Ni kenya na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo pekee ambazo bado hazijawasilisha  majini ya wabunge wao tisa watakaowawakilisha katika bunge la Afrika Mashariki la EALA.

Sheria za eala elfu mbili kumi na moja zinasema kuwa bunge mpya lichaguliwe katika siku tisni kabla ya bunge linahudumu kukamilika.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here