“Nilikeketwa kwa hiari ila madhara makuu” mwanaharakati afunguka

0
12

Mashirika mbalimbali ya serikali na yale yasiyo ya serikali yametoa tahadhari kwa wazazi kuwa macho msimu huu wa likizo ndefu ili kuzuia ukeketaji. Takwimu za serikali zinaonyesha kwamba tohara kwa mtoto msichana katika kaunti za Kisii na Nyamira inazidi kuongezeka kwa kasi.

Katika kijiji cha Nyaronde maeneo ya Nyanzionge eneo bunge la Borabu, Gladys Orina anajitayarisha kwenda kwenye hafla ya kutoa mafunzo kwa akina mama wakongwe ambao mara nyingi hutumika katika kukeketa watoto wasichana Hususan musimu huu wa likizo ya Disemba.

“Mimi nilipashwa tohara kwa hiari kwa kuwa ni miongoni mwa mila zetu. Ila haikuwa rahisi sana kwa kuwa mimi pamoja na wenzangu tuliokeketwa tulihisi uchungu sana na kuvuja damu nyingi jambo ambalo hatukufurahia,” Gladys Orina- Mwathiriwa wa ukeketaji.

Orina ni mwanamke anaye julikana kote Kisii na nyamira kwa juhudi zake za kuhamazisha jamii  dhidi ya ukeketaji kutokana na madhila aliyopatana nayo akiwa  na umri mdogo.

“Kutokana na utafiti bado tunaegemea kwenye tafitiza mwaka wa 2014 na ambazo zinaonyesha kuwa idadi hii ya ukeketaji bado ipo katika kiwango cha juu cha asilimia 84,”Kutwa Kinyerere -afisa bodi ya kukabiliana na ukeketaji.

Mara nyingi gladys hutembelea vikundi vya akina mama Kisii na Nyamira mara kwa mara ili kutoa hamasisho kabambe. Licha ya jitihada zake, takwimu za kutoka bodi ya kitaifa ya kupambana na  ukeketaji nchini ikionyesha kuwa ukeketaji ungali katika kiwango cha juu cha asilimia 84 eneo nzima la kisii.

Wasiwasi mkubwa wa wazazi kwa wanao wa kike katika maeneo hayo kwa sasa ni likizo ndefu ijayo ya miezi miwili. aidha washikadau wametoa wito kuungwa mkono wanapotekeleza wajibu wao vijijini.

Na Juliet Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here