Hali tata yaikumba bahari Hindi

0
2

Shughuli za binadamu zaendelea kuhitilafiana na mazingira ya bahari Hindi kila uchao kutokana na utupaji wa taka kiholela na ukataji wa miti ya mikoko, hali ambayo huathiri viumbe baharini kama vile Samaki.

Uhamasisho kuhusu utunzaji wa mazingira umechukua mkondo mwingine huku wasanii wakijitosa nyanjani kutoa hamasa kwa umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira. Sanaa hiyo inaendeshwa na kikundi cha Jukwaa Arts kuelezea umma kwa ufasaha ili kuhamasisha wakazi hasa wa Pwani kutilia mkazo haja ya kutunza mazingira.

Kikundi hicho kinatumia muziki, uigizaji na sanaa ya michoro baada ya kupata mafunzo ya kisayansi kutoka kwa wataalamu wa mazingira.
“Jamii hawataelewa vitabu vya sayansi na hata hawatajua watazipata wapi. Lakini hii sanaa tumeitengeneza na pia hatubakishi tu hapa kwa ‘theatre’ kwa sababu pia jamii haitakuja kwa ‘theatre’ lakini tunawapelekea kwao mashinani.” Carolyne Ngorobi, mwelekezi wa Jukwaa Arts alisema.

“Ile kazi ambayo tumefanya hapa ni muhimu sana kwa sbabu huu ujumbe tumeufikisha mbali sana, kwa watu ambao hawaelewi hizo takwimu za mazingira na tabianchi ambazo Wanasayansi hutoa.” Mary Favour, mwigizaji wa Jukwaa Arts alisema.

Siku chache zilizopita kulikuwa na hasara kubwa ya kupoteza Samaki wengi sana kutokana na uchafuzi wa ziwa Viktoria. Kumaanisha kwamba haja ya kuhifadhi mazingira na hasa viungo vya maji ni jukumu letu sisi sote na kutakuwa na manufaa kwetu na hata kwa wanyama waishio majini.

Na Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here