“Daktari wa Cuba hapa nchini analipwa mara kumi zaidi ya daktari mwenyeji” KMPDU

0
3

Chama cha madaktari nchini KMPDU ukanda wa kaskazini mwa bonde la Ufa, kinaitaka serikali ya kitaifa na serikali za kaunti kushirikiana kununua vifaa na dawa pamoja na kuwaajiri madaktari zaidi. Madaktari hao walikuwa wakizungumza katika mkutano wao wa mwaka mjini Eldoret.

Chama hicho sasa kinaitaka serikali kuu kuwaajiri madaktari kutoka humu nchini badala ya kuleta madaktari kutoka nchi za nje, kulingana nao ni gharama kubwa kulipa madaktari kutoka ughaibuni kuliko kuwalipa waliomo nchini.

“Tunataka kujua hawa madaktari kutoka Cuba wanalipwa pesa ngapi kwa sababu inaaminika kuwa pesa ambazo zinalipwa daktari mmoja kutoka nje zinaweza kulipa madaktari zaidi ya kumi hapa nchini.”

Muungano huu pia umeitaka serikali za kaunti kuhakikisha kuwa wanaleta vifaa za matibabu na dawa katika hospitali ndiposa Wakenya waweze kusaidika wakati ambapo wanatafuta matibabu.

“Tunaziomba serikali za kaunti na magavana kuhakikisha hospitali zetu zinapata viffaa ya matibabu na dawa kwa wakati.”

Madaktari hawa ambao walikuwa wakizungumza mjini eldoret katika mkutano wao wa kila mwaka wamesema kwamba, wakati wa kampeni kabla ya uchaguzi wa tarehe tisa Agosti kuna ahadi zilizoahidiwa na serikali ya kumi na tatu za kuimarisha sekta za afya na sasa wanaiomba serikali kutekeleza ahadi hizo.

Afya ni swala la kimsingi ndiposa madkari hawa wamejitolea kuzungumza kwa niaba ya Wakenya na wanaitaka serikali kuipea sekta kipaumbele.

Na Faith Njerwe

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here