
Wiki ya kwanza ya kongamano la mabadiliko ya tabia nchi imekamilika nchini Misri, huku washiriki zaidi ya elfu hamsini wakipata nafasi ya kupumzika jana kabla ya mazungumzo kuanza tena leo hii inasemekana kuwa kuandaa kongamano la aina hii sio jambo rahisi kwani kunahitaji ushirikiano wa zaidi ya mataifa mia moja tisini na wanachama wa umoja wa mataifa.
Huku wiki ya kwanza ya kongamano linaloendelea la kuangazia mabadiliko ya tabia nchi likikamilika mjini Egypt washiriki zaidi ya elfu hamsini walipumzika hapo jana kisha kuanza tena leo hii ikiwa ni wiki ya pili na ya mwisho ya kongamano hili.
Kuandaa kongamano la aini hii linalowaleta pamoja washiriki kutoka nchi mia moja tisini tofauti, wakiwemo viongozi wa mataifa, wanaharakati wanahabari na hata wafanyi biashara sio kazi rahisi.
Mmoja wa wale wanaosimamia kongamano hili ni mkenya, Cecilia Kinuthia Njenga, ambaye ni mmoja wa viongozi katika kongamano hili ni mkurugenzi wa shirika la umoja wa mataifa linaloangazia mabadiliko ya tabia nchini. Alielezea kwa kina jinsi maandalizi hayo na usimamizi wa kongamano hili yanavyofanyika.
“Kuandaa mkutano wa aina hii si rahisi, mkutano huu unatakiwa kuleta watu Zaidi ya elfu hamsini kutoka nchi tofauti tofauti.”
Cecilia alisema kuwa amesafiri nchini Misri mara kadhaa kwa ajili ya kongamano hili na shughuli zingine, aliongezea pia alikuwa nchini misri kwa takriban mwezi moja kabla ya kuanza kwa ajili ya matayarisho na mipango ya hafla hii inayoendelea.
“Nimekuwa nchini misri kwa takriban mwezi mmoja kwa maandalizi ya kongomano linaloendelea na nimejifunza mengi kuhu nci ya msri kwa muda mchache ambao nimetangamana nao.”
Na sasa wiki ya pili na ya mwisho inaanza, wiki ambayo itakuwa na shughuli mingi zaidi kwani mawaziri na viongozi watafika hapa kwa mazungumzo ya mwisho.
Na Marion Wafula