
UCHAFUZI WA ZIWA VIKTORIA
Uvundo na uchafu katika Ziwa Viktoria unawakosesha wanamazingira amani. Wanamazingira hao pamoja na viongozi wa kaunti ya Homabay wametaka washikadau kwenye kongamano la kudhibiti mabadiliko ya tabianchi inayoendelea nchini Misri almaarufu COP 27 kuzingatia suala hilo.
“There is a lot of pollution that has taken place in the lake and right now people are counting millions and millions of losses due to the death of fish in the lake and especially in the fish cages. But we should not only look at the fish cages, we should also look at the aqua plants and several other animals that are depending on the water body for survival.” One of the environmentalists said (Willis Omulo).

“Kuna uchafuzi mkubwa ambao umetokea ziwani na sasa hivi watu wanahesabu mamilioni na mamilioni ya hasara kutokana na vifo vya samaki ziwani na hasa kwenye mabwawa ya samaki. Lakini tusiangalie tu mabwawa ya samaki, pia tuangalie mimea ya majini na wanyama wengine kadhaa ambao wanategemea maji kwa ajili ya kuishi.” Mmoja wa wanamazingira alisema.
Wiki iliyopita wafugaji wa Samaki katika ufuo wa Kamolo eneo bunge la Karachuonyo walipoteza Samaki wenye thamani ya takriban shilingi milioni mia moja kutokana na uchafu wa mazingira, hali ambayo kulingana na shirika la utafiti KMFRI ilisababishwa na ukosefu wa hewa safi majini.
“Having Lake Victoria in our country, the greatest part of the lake and is affected by pollution, we are told now fish are dying and that is basically due to effects of climate change and we are seriously concerned as scientists and we are asking people, the government, institutions to come together so that we strengthen the issue of fighting the impacts of climate change.” One of the scientists said. (Clifford Omondi)
“Kuwa na Ziwa Victoria katika nchi yetu, sehemu kubwa ya ziwa, na limeathiriwa na uchafuzi wa mazingira, tunaambiwa sasa samaki wanakufa na hiyo kimsingi inatokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na tuna wasiwasi mkubwa kama wanasayansi na tunawaomba watu, serikali, taasisi mbalimbali kuungana ili tuimarishe suala la kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.” Mwanasayansi mmoja alisema.
Serikali ya kaunti ya Homabay ikiongozwa na Gavana Gladys Wanga sasa imeanza mipango ya usafi ziwani kwa kushirikiana na washikadau wa mazingira.
“So, today’s message is let everyone take responsibility especially for our lake because if we dump in our lake, we will soon not have any fish to write home about because we will alter the environment for our fish,” Homabay Governor Gladys Wanga said.
“Kwa hiyo, ujumbe wa leo ni kila mtu achukue jukumu hasa kwa ziwa letu kwa sababu tukitupa taka katika ziwa letu, hivi karibuni hatutakuwa na samaki wa kuandikia nyumbani kwa sababu tutabadilisha mazingira ya samaki wetu.” Gavana wa Homabay Gladys Wanga alisema.
Na Calvin Angatia