Shughuli za kuondoa mashtaka dhidi ya naibu  wa rais Rigathi Gachagua inasikizwa mahakama  ya milimani. Gachagua pamoja na watu wengine walishtakiwa kwa ufisadi na uhalifu wa kiuchumi. Upande wa mashtaka unasema hauwezi kuendelea na kesi hiyo kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Naibu wa rais Rigathi Gachagua ni baadhi ya waliochunguzwa na tume ya ufisadu eacc na kupatikana na kesi za ufisadi na kushtakiwa mahakamani. Kesi yake iko katika kikao ili kuondolewa baada ya kukosa ushahidi wa kutosha.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji leo jumatano asubuhi aliomba kuondoa mashtaka ya ufisadi ya shilingi bilioni 7.3 dhidi ya naibu rais Rigathi Gachagua na watuhumiwa wenzake.

Haji ameiambia mahakama kuwa idara ya upelelezi wa jinai, DCI haikutoa ushahidi wa kutosha wa kesi hiyo hali iliyomlazimu kuchukua hatua hiyo.

Mahakama itatoa uamuzi kuhusu kuondolewa kwa kesi ya ufisadi dhidi ya naibu rais Rigathi Gachagua na wengine.hii ni baada ya upande wa mashtaka kuiomba mahakama kuondoa kesi kwa misingi kuwa uchunguzi haukukamilishwa.

Gachagua anatuhumiwa kwa uhalifu wa kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujipatia mali ya umma kwa njia ya udanganyifu, kujipatia mali ya uhalifu, kupanga njama ya kutekeleza ufisadi, mkinzano wa maslahi na ulanguzi wa pesa.

 mkurugenzi wa mashtaka ya umma anasema kesi hiyo haiwezi kuendelea ilivyo. Afisa mkuu wa upelelezi Obadia Kuria ameieleza mahakama kuwa ushahidi uliopo hautoshi kuwafungulia washukiwa kesi.

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili mkuu Kioko Kilukumi ulipongeza hatua hiyo ukisema kuwa watuhumiwa walishtakiwa bila ushahidi wa kutosha.

Taarifa za kiapo za afisa anayechunguza kesi hiyo zilimlaumu aliyekuwa mkurugnzi wa DCI George Kinoti kwa kumshinikiza afisa huyo kuwashtaki washukiwa hao licha ya ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here