Kero la wizi wa mifugo, mwanaume mmoja apigwa risasi na kuwauwa

0
3

Wizi wa mifugo katika kaunti ya samburu umekuwa ni kero kwa wakaazi wa kaunti hiyo. Kero hilo la wizi wa mifugo limekithiri hii ni baada ya wezi hao kuvamia kijiji cha Lolmolog, kuiba mbuzi zaidi ya 240 na kutoweka nao.
“Wezi hao waliweza kuingia ndani ya boma, hili boma lina milango kadha. Waliingia mwendo wa saa tano saa sita hapo, wakavunja panda la mbuzi na kutoweka na mbuzi zaidi ya 240,” Meule Lodung’okio, mwathiriwa wa wizi huo alielezea.

Wakaazi hao wanasema kuwa walihofia kutoka nje kuwakabili wavamizi hao ila waliwazuia kutoka nje kuwasaidia mifugo hao wasitoweke na wezi hao. Waliona ni heri wakae ndani kwa sababu tayari mwanamume mmoja alikuwa amepigwa risasi na wezi hao na kuachwa hali mahututi.

“Watu walikuwa wamezuiliwa ndani ya nyumba zao, hakuna mtu angetoka nje, kama watu wangejaribu kutoka wameuwawa huku,” Joseph Longongo, mwenyekiti wa nyumba kumi alisema.

Wizi huo umewaathiri wakazi katika kijiji hicho, wakisema kuwa waliwategemea mifugo hao kupata mapato na fedha za kuwakimu maishani ikizingatiwa uchumi umekuwa mbaya sana humu nchini.

“Nina wasichana wanne, mmoja yupo chuo kikuu, mwingine yupo chuo cha mafuzo ya kiufundi, mwingine yupo shule ya upili na mwingine yupo shule ya msingi. Watoto hao wanahitaji karo ya shule ilipwe, nasi pia huwa tunakosa chakula cha kula. Ninahitaji pesa kuwakimu watoto hawa, kwa sasa hamna namna ya kupata hiyo pesa kwa sababu wameituibia mbuzi wetu,” Bi. Lodung’okio alielezea huku amesikitishwa.

Wakazi hao wameirai idara ya usalama kuingilia kati suala hilo, kuhakikisha kuwa wezi hao wanafuatiwa na kukamatwa na mifugo hao kuregeshwa. Wameimba idara ya usalama kuingilia kati na kuwahakikishia kuwa wanapata mifugo wao walioibiwa.

“Tunajua kuwa waziri wa usalama yupo karibu kutembelea kaunti ya samburu mnamo tarehe 18. Yale tunayotarajia kutoka kwake ni kutuahidi kuwa mbuzi wetu wataregeshwa. Tumewahimiza watu wetu wakae kwa amani mpaka serikali itakapotoa mwongozo. Sisi kama wazee wa samburu tutakaa na yeye tuzungumzie hilo suala tupate kuwa na hakikisho kuwa mali yetu itarudishwa,” mmoja wa wazee kwenye kijiji hicho cha Lolmolog aliwakikishia wakazi hao.

Inspekta generali mkuu wa polisi mteule, japeth koome akihojiwa jana na kamati ya bunge la kitaifa aliahidi kukabiliana na wezi wa mifugo kwa kusema kuwa yoyote atayepatikana na hatia atafungwa kifungo cha maisha gerezani.

Na James Chacha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here