Wazazi na wanafunzi wa shule ya upili ya Nalondo waandamana

0
12

Wanafunzi wa shule ya upili ya Nalondo kaunti ya Bungoma pamoja na wazazi wa shule hio wameshiriki katika mmandamano leo hii baada ya mwalimu mkuu kuitisha fedha za kugharamia marekebisho ya bweni lililochemeka kwa mkasa wa moto uliosababishwa na umeme.

Wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana ya nalondo katika kaunti ya Bungoma wameshiriki katika maandamano baaada ya mwalimu mkuu kuwaamrisha kutoa shillingi elfu nne ya marekebisho ya bweni lililochomeka.inaaminika kuwa chanzo cha mkasa wa moto umeme na si wanafunzi hao.

Wazazi wa shule hii wamelalamikia kuitishwa pesa kila mara japo kuwa hawaoni maendeleo yoyote katika shule hiyo. Na sasa wanaitaka wizara ya elimu kuingililia kati na kutoa mwalimu huyo kwenye kiti.

Wazazi wenye ghadhabu walikataa kuhudhuria mkutano uliokuwa umepangawa na walimu wa shule hii ukiongozwa na mwalimu mkuu wakimtaka mwalimu huyo kuelezea jinsi kila peni walio lipa kwenye shule hii ilivyo tumika

Josephine Simiyu ambaye ni mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajiwa kuanza mtihani wa kitaifa wiki tatu kutoka sasa, amelalamikia wanafunzi kurudishwa nyumbani mara kwa mara ili kuleta karatasi za kuchapisha mitihani hata baada ya kukamilisha karo.

Akizungumuza na wazazi, mwalimu mkuu alidai kuwa anafanya hayo yote kwa maslahi ya wanafunzi ili kuwalinda. Aliongeza pia bweni hilo litatengenezwa muda usiokuwa mrefu kutoka sasa.

Kwa upande mwingine, wanfunzi wa shule hii walilalamika kuwa mwalimu mkuu kuwatusi na kuwalaani kila siku katika gwaride na walitishia kuwa iwapo wizara ya elimu haitamtoa kwenye shule hii watazidi kufanya maandamano ya kumtoa wenyewe kwa wenyewe

Wazazi   wamelalamikia waziri mpya wa elimu Ezekeiel Machogu na serikali ya rais William Ruto kuingililia kati ili kutatua swala hili.

By Marion Wafula.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here