Inspekta mteule Japheth Koome apigwa msasa, aahidi kukabiliana na utovu wa usalama

0
2

Akifika kwenye kamati ya bunge la kitaifa kupigwa msasa juu ya mipango yake ya utendakazi punde utakapoanza kazi rasmi, inspekta mkuu wa polisi, Japeth Koome aliteuliwa na rais William Ruto kusimamia kitengo hicho cha idara ya polisi. Ameulizwa maswali kuhusiana na idara hiyo ya polisi, akisema kuwa atajisatiti kuhakikisha kuwa anafanya marekebisho kwenye idara hiyo.

Inspekta huyo wa polisi amesema kuwa alijiunga na chuo kikuu cha polisi kusomea uhandisi baada ya kuwa afisa wa polisi, akisema alijitolea yeye mwenyewe kufanya hivyo. Amefaa kuelezea waziwazi kama madai ya yeye kujiunga na chuo kikuu yalikuwa ya kweli baada ya kuwa kwenye kikosi cha polisi.

“Mpango ulikuwa, hii ilikuwa kujitolea wala si kulipwa. Mbinu ilikuwa kupitia huo mpango na hatimaye kujiunga na kikosi cha polisi. Wewe ni mkurugenzi mahali au wewe ni mbunge, utakuwa na fikra ya idara ya usalama, hiyo ndiyo ilikuwa mbinu lakini huo mpango haupo kwa sasa’, inspekta mkuu wa polisi mteule,” Japheth Koome alielezea.

Wizi wa mifugo umekuwa ni chanzo cha wengi kupoteza mali na mauji ya kiholela. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaojihusisha na wizi wa mifugo akisema kuwa yoyote atakaye patikana na hatia atafungwa maisha gerezani.

“Wale ambao wanajihusisha na wizi wa mifugo watahukumiwa kifungo cha maisha, na hilo litachangia sana kumaliza wizi wa mifugo. Hayo yatatimia iwapo mtaniidhinisha kwenye mamlaka hayo niliyoteuliwa ili tufanye kazi pamoja na tumalize hili jambo kabisa. Vijana wanaojihusisha na wizi wa mifugo, tunafaa kuwapa mafunzo kwenye vyuo vya kiufundi wapate kujisaidia’, aliendelea kujitetea jinsi atavyofanya kazi punde atakapoanza kazi.

Asilimia 98 ya maafisa wa polisi wameonyesha kuwa wazalendo na wachapakazi, akiahidi kuwa asimia 2 iliyobakia ya maafisa wa polisi wataambatana na wenzao.

“Nina imani ya utendakazi kwa usaidizi wa hii kamati na maafisa wa polisi wenzangu. Maafisa wa polisi ni wazuri humu nchini, asilimia 98 ni wazalendo na wachapakazi lakini asilimia 2 ambayo imebakia nina uwezo wa kuibadilisha,”alisema.

Amedhibitisha kuwa unywaji wa pombe na utumizi wa mihadharati mengine imekuwa ni chanzo cha vijana wengi kukosa mwelekeo katika maisha. Amesema atachukua hatua kwa kuhusisha idara zinazohusika ili kukomesha unywaji wa pombe na utumizi wa mihadharati baina ya vijana.

“Suala la unywaji wa pombe na utumizi wa mihadharati linafaa kuzingatiwa kwa kina zaidi
kwa sababu iwapo hatupo makini tutapoteza vizazi vijavyo. Mwenyekiti na kamati nzima,
nikiidhinishwa kwa uteuzi wangu sitangoja mkurugenzi wa kitengo cha kukabiliana na
mihadharati aje kwenye ofisi yangu bali mimi mwenyewe nitaenda kwake kuzungumzia hili
swala,” alielezea.

Na James Chacha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here