
Kingozi wa chama cha wiper, Kalonzo Musyoka ameonekana kukosa msimamo dhabiti kisiasa huku akimtaka rais William Ruto kumhusisha katika shughuli za kusambaza chakula cha msaada aidha Kalonzo amesema yuko tayari kushirikiana na Ruto na serikali yake.
Kinara wa chama cha Wiper ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa upinzani na mrengo wa Azimio la Umoja, ameonekana kuvuta pande zote kuhusu mustakabali wake wa kisiasa licha ya kusisitiza atakuwa upande wa upinzani, kiongozi huyu bado anaendelea kutafuta ushirikiano wake na rais William Ruto na serikali yake.
Kalonzo alisema kuwa atazididi kuwa nduguye rais William Ruto kwa sababu rais Ruto alisema hivyo alipokuwa Kitui.
Akizungumza alipohudhuria ibada siku ya jumapili kaunti ya Kajiado, Kalonzo alisema kuwa anataka kuhusishwa katika shughuli za kusambaza chakula cha msaada katika kaunti zilizoathiriwa na ukame.
Kauli yake Kalonzo ikionekana kuwa mojawapo ya sababu kutaka kujihusisha na serikali ya rais William Ruto ambaye mara kwa mara ameonekana kumnyoshea mkono wa aheri na kutaka ajiunge na serikali yake.
Kalonzo aliongezea kuwa yuko tayari kutoa msaada wa aina yoyote iwapo ataulizwa na serikali ya rais William Ruto lakini bado atasalia upande wa upinzini aliahidi wakenya na wanachama wa mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya.
Aidha Kalonzo amemtaka rais William Ruto kumhusisha katika majadiliano ya kutatua mgogoro ulioko kati ya serikali na marubani wa shirika la kitaifa la ndege, alisema kuwa yuko tayari kumsaida waziri Kipchumba Murkomen.
Hata hivyo Kalonzo amepinga mara kwa mara wazo la kujiunga na serikali ya rais William Ruto akidai kuwa yeye ni mmoja wa viongozi wa upinzani.
Na Marion Wafula