Barabara Bungoma yazua balaa

0
61

Wakaazi wa mjini bungoma walishuhudia ajali katika barabara kuu ya Musikoma-Kanduyi. Ajali hii ilihusisha gari la aina ya tuktuk na gari la kibinafsi. Bungoma ni baadhi ya miji inayo shuhudia ajali za namna hii.

Ukiukaji wa alama za barabarani haswa zile za trafiki umekuwa chanzo kikuu cha ajali mingi zinazoshuhudiwa haswa kwenye barabara kuu mijini. Bungoma ni baadhi ya miji ambazo zimeshuhudia ajali za namna hii.

Hapo jana mwendo wa saa nne asubuhi, ajali ilitokea kwenye barabara ya dual carriage way ya Musikoma-Kanduyi mjini Bungoma. Ajali hiyo ilihusisha tuktuk na gari la kibinafsi. Inadaiwa kuwa dereva wa gari alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi ili kupita tuktuk kisha akagonga tuktuk hiyo na kuanguka mtaroni kando ya barabara.

Inasemekana kuwa kumekuwa na tabia ya kupuuza sheria za trafiki kwenye barabara hiyo ya dual carriage na kusababisha ajali. Waendeshaji wa bodaboda wamelalamikia uvunjaji holela wa kanuni za barabara na kupuuza alama za trafiki huku mwendo kasi ikiwa chanzo kikuu cha ajali.

Mbali na hayo, mwendeshaji bodaboda mmoja alionekana akiendesha pikipiki leni isiyo yake, huku akidai kuwa bei ya mafuta kupanda ilichangia kwani hakuwa na mafuta ya kutosha kurudi kwenye mzunguko ili achukue leni yake.

Mkaazi mwingine alidai kuwa waendeshaji  bodaboda wasitumie kupanda kwa bei ya mafuta  kama sababu ya kuvunja sheria za barabara.

Wito umetolewa kwa watumizi wa barabara, wanatakiwa kuelimishwa kuhusu matumizi sahihi ya barabara na kuzingatia sheria za trafiki ili kuepuka maafa zaidi kwenye barabara zetu.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here