Nyota chipukizi: Alejandro Garnacho

0
13

Mshambulizi chipukizi wa manchester united Alejandro Garnacho ameanza kufuata nyayo za mshindi mara tano wa tuzo la ballon d’or, Cristiano Ronaldo licha ya kuwa raia wa taifa la Argentina sawa na Lionel Messi ambaye amekuwa mshindani mkuu wa Ronaldo.

Garnacho alifunga bao lake la kwanza kwenye kikosi kikuu cha Man United baada ya kumegewa pasi na nyerezi Cristiano Ronaldo katika mechi 9 ya mwisho ya mashindano ya europa kati ya  Real Sociedad na Man United siku ya alhamisi na kuipa United alama tatu na kuisaidaidia United kuimaliza kwenye nafasi yua pili katika hatua ya makundi.

Kuzaliwa: 1 July 2004 (age 18 years), Madrid, Spain
Timu: Manchester United FC. (#49 / forward), more
Urefu: 1.8 m
Nchi: Argentine, Spanish
Uzani: 80 kg
Ligi ya Uropa…….

Argentina u 20……..4m…….1g

Man u 23…………………4m…….4g….1a

Man u u19……………….7m……2g

Man u18………………….16m…..7g

Mshambulzi huyo alikuwa wa mwisho kutajwa kwenye kikosi cha Argentina kwa ajili ya mashindano ya Kombe la dunia yatakayoandaliwa kule Qatar mwezi huu.  Garnacho  atacheza pamoja na wachezaji mashuhuri kama vile mshindi mara saba wa tuzo la Ballon D’or Lionel Messi, Paulo, Dybala, Julian Alvarez wa Man City na mchezaji mwenzake wa Man United Lisandro Martinez.

Na Brian Simiyu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here