Viongozi, Wajir walalamikia kutengwa katika uteuzi licha ya kusimama naye Rais Ruto

0
10

Viongozi kutoka kaunti ya Wajir wametilia doa orodha ya walioteuliwa na rais William Ruto kuchukua nafasi za makatibu wa kudumu wizara ishirini na moja nchini. Viongozi hao wanalalama kuwa kaunti ya Wajir imeachwa nje katika uteuzi wa serikali ya rais Willim Ruto licha kusimama naye katika uchaguzi Agosti 9.

Wakiongozwa na mbunge wa Wajir kaskazini ibrahim saney na mwenzake wa Tarbaj Hussein Barre, walidai kuwa walishinda UDA katika eneo la azimio hivyo basi eneo hilo lilifaa kuzingatiwa katika uteuzi wa mtendaji na ubunge.

“Tunaona hali ambapo tunaadhibiwa kwa kuwa na rais. Tunahisi chama chetu kinatuadhibu kwa kusimama na rais,” alisema Barre.

Tume ya utumishi wa umma (PSC) ilituma majina 250 kwa rais Ruto ambapo mkuu wa nchi aliwateua makatibu wakuu 51 na kubakiza sitawaliohudumu chini ya utawala wa rais mstaafu Uhuru Uenyatta.

Miongoni mwa waliozuiliwa ni naibu waziri wa ugatuzi julius korir ambaye sasa atahudumu kama wizara ya mambo ya nje ya masuala ya baraza la mawaziri chini ya afisi ya naibu rais, waziri wa ukanda wa kaskazini belio kipsang atarejea katika hati ya elimu, waziri wa nyumba charles hinga ataendelea kuhudumu katika idara hiyo. .

Baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Wajir wametoa malamishi ya kuachwa nje ya serikali ya kumi na tatu inayoongozwa na rais William Ruto.viongozi hawa  wametoa malalamishi haya baada ya kukosa kwenye orodha ya mawaziri ishini na moja waliochaguliwa.

Walisema kuwa wanaheshimu maamuzi ya rais William Ruto lakini wanalamikia kusahaulika hata baada ya kuwa waaminifu na kusimama na yeye kabla ya uchaguzi wa tarehe tisa agosti.

Kiongozi mwingine wa chama cha UDA alidai kuwa wanachama wa upinzani wanapewa vyeo vikubwa kama makatibu wakuu na uwaziri wakati watu waliopigia rais William Ruto hawana nafasi yoyote katika serikali yake

Viongozi hawa wanatarajia kuwa malamishi haya yatafikia rais William Ruto na yatashughulikiwa.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here