Kiswahili kutamba Kenya; bunge launga mkono kuzinduliwa kwa baraza la kiswahili

0
13

Wabunge wametoa hoja ya kuunga mkono kuzinduliwa kwa baraza la kitaifa la kiswahili. Wabunge hao wamechanjia hoja hiyo ilitolewa na mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan, wakipendekeza uzinduzi huo ambao utaleta umoja na utangamano kote ulimwenguni. Kulingana na wabunge hao, kuzinduliwa kwa baraza la kiswahili kutawezesha uelewano uwepo kwa urahisi. Kigezo muhimu cha lugha ni kupata kueleweka kwa wepesi, wakisema lugha ya kiswahili ina uelewa wa haraka.

“Mimi kama daktari bwana spika, mara nyingi unapoongea na mgonjwa akuelezee ugonjwa wake kwa lugha ambayo unaweza kuielewa. Wengine unajua wanapoongea wanaweza wakatumia lugha ambayo haieleweki,” mbunge mmoja alitoa hoja ya kuunga mkono hoja hiyo ya kuzinduliwa kwa baraza la kiswahili.

Watalii na wananchi wa mataifa ya kigeni watapata kufunzwa lugha hiyo ya Kiswahili, kama ilivyo kwenye mataifa mengine wakati wakenya huenda kwenye mataifa hayo kwa shughuli mbalimbali.

“Kuzinduliwa kwa baraza la kiswahili humu nchini, itawalazimu hata wale wanaotoka nchi za ughaibuni ambao wanafanya kazi humu nchini kuhakikisha kuwa wanaenda shuleni wajifundishe lugha ya kiswahili kama ilivyo desturi ya wakenya wengi ambao wanatafuta nafasi za kazi katika nchi ambazo hazizungumzi kiingereza na inabidi kwamba wakifika kule wanajifunza lugha zao,” mbunge wa eneo bunge la kimilili alieleza bunge.

Uzinduzi wa baraza hilo la kiswahili utahakikisha kuwa lugha ya kiswahili inawaunganisha watu na huo ndio umuhimu wa lugha katika jamii yoyote ile.” Lugha ni muhimu katika jamii yoyote ile. Lugha inavyokuzwa inasaidia sana kuunganisha jamii, pia inaendeleza vyema masuala ya biashara,” mbunge mwingine alisema.

Utumizi wa lugha ya kiswahili utahakikisha kuwa utatoa utafauti wa kikabila ambao umekuwa ukishuhudiwa nchini.

“Leo hii katika taifa letu la kenya, tuna lugha ama lugha za kikabila zaidi ya 45. Hivyo basi zinazidi kutia mambo ya kikabila iwapo hatutachangua lugha moja ambayo itatuunganisha. Kwa hivyo, tukiweza kukuza lugha hii ya kiswahili, mambo ya kikabila, tofauti za kikabila zitaweza kupungua,” mbunge mwingine alisema.

Wabunge vile vile, wamesema uzungumzaji wa lugha ya kiswahili utakuwa na watu wengi nchini baraza hilo litakapo zinduliwa. Lugha hiyo ikipewa fursa ya kuzungumzwa nchini, watu wengi watapata kuzungumza lugha hiyo na vilevile itaenezwa kwa vizazi zijavyo.

Hoja hiyo ya kamati ya utamaduni na utalii wa kuanzisha baraza la kiswahili nchini itaweka mikakati, mbinu na sera za kuimarisha na kuendeleza lugha ya kiswahili nchini. Iwapo mswada huo wa kupitishwa kuzinduliwa kwa baraza la kitaifa la Kiswahili, Kiswahili kitatukuzwa nchini hivyo basi lugha hiyo kupewa hadhi inayofaa kama lugha nyingine kama kiingereza.

Na James Chacha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here