Jopokazi la CBC laendelea kukusanya maoni katika kaunti mbali mbali nchini

0
17

Ni mwezi mmoja sasa baada ya Rais William Ruto kuteua jopokazi la elimu ili kupata mwelekeo wa sekta mbalimbali za elimu, kama vile mtaala wa CBC. Vikao vya jopokazi hilo vilianza hapo jana katika kaunti kumi ili kupata maoni kutoka kwa walimu, wazazi na wanafunzi kuhusu mtaala wa CBC. Maoni tofautitofauti yaliyotolewa katika kaunti mbalimbali.

Akizungumza katika shule ya kitaifa ya Lodwar kaunti ya Turkana, Profesa Raphael Munavu amewashauri wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuwasilisha maoni yao kuhusiana na mtaala wa CBC.

Wanakamati hao wamegawanywa katika vikundi kumi ambavyo vitazuru kaunti tofauti kabla ya kufunga kongamano la ushiriki wa umma tarehe 11 Novemba mwaka huu.

Vikao vitafanyika ifuatavyo;


Alhamisi tarehe tatu Novemba
 Mombasa – Coast Girls
 Makueni – Makueni Boys
 Nyeri – Nyeri High
 Elgeyo Marakwet – Tambach Teachers College
 Bungoma – St. Teresa Sio Secondary
 Nyamira – Sironga Girls
 Homa Bay – Homabay Boys
Ijumaa tarehe nne Novemba
 Isiolo – Isiolo Girls
 Wajir – Wajir High
 Laikipia – CDF Hall Nanyuki

Jumatatu tarehe saba Novemba
 Kilifi – St. Thomas
 Kitui – Kitui Multipurpose Hall
 Bomet – Tenwek Boys
 Kirinyaga – Kerugoya Girls
 Trans Nzoia – St. Monica Girls

 Kakamega – kakamega High
 Kisii – Kisii University
Jumanne tarehe nane Novemba
 Meru – Meru TTC
 Garissa – Nep Girls
 Baringo – KSG Baringo
Jumatano tarehe tisa Novemba
 Lamu – Mokowe Arid Zone Primary
 Embu – University of Embu
 Murang’a – Murang’a TTC
 West Pokot – Nasokol Girls
 Narok – Ole Tipis Girls
 Nandi – Kapsabet Girls
 Siaya – Nyamira Girls
Ijumaa tarehe kumi na moja Novemba
 Tana River – Hola Primary
 Machakos – Machakos Girls
 Tharaka Nithi – Chuka University
 Kiambu – Chania Boys
 Uasin Gishu – Uasin Gishu High
 Kajiado – Umma University
 Vihiga – Moi Vihiga Girls
 Kisumu – Kisumu Girls
 Nairobi – University of Nairobi
 Nakuru – Nakuru Girls

Na Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here