Je, unafahamu mazuri yaliyoletwa na “Handshake”?

0
17

Muungano wa mwaka elfu mbili kumi na nane kati ya rais wa zamani uhuru kenyatta na kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga ulisababisha madhara zaidi kuliko wema kwenye uchumi wa Kenya. Haya yamedhihirika baada ya kufuatilia maoni ya wakaaji wa kaunti ya bungoma waliosisitiza utawala wa ruto usiruhusu muungano wa aina hiyo kuhakikisha serikali yake ina upinzani ili sauti ya watu.

“Maisha ya handshake yalilileta madhara makubwa haswa kwa biashara hizi ndogo. Bei ya kila kitu kilipanda na kusababisha mzozano kati yetu na wanunuzi, tunaomba serikali mpya ambayo imeingia uongozini itutengenezee uchumi.” Mkaazi wa Bungoma alisema

Mkazi mwingine ambaye bado katika kaunti ya Bungoma alikiri malalamiko yake akisisitiza jinsi gharama ya maisha ilivyopanda baada ya muungano huo. Waliongezea kwa  maisha yalikuwa magumu kwa mwanchi wa kawaida hasa watu wa boda boda, mama mboga na wafanyabiashara wengine wadogo.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here