
Jukwaa mpya la “golive africa” limevumbuliwa ili kusaidia mashabiki wa televisheni ya Tandao kupata kipindi chochote kwenye televisheni hiyo. Mkurugenzi mkuu wa runinga ya Tandao Robert Wanyonyi ameeleza kwa ufasaha jinsi mtu anaweza kupata jukwa hili na jinsi ya kupata kipindi chochote kinachotoka moja kwa moja kwenye televisheni.
Akizungumza wakati alipo kuwa akiwaarifu mashabiki wake, mkurugenzi mkuu wa runinga ya Tandao Robert Wanyonyi alielezea jinsi jukwaa mpya iitwayo golive africa inafanya kazi. Jukwaa hili limewekwa ili mashabiki kupata programu zozote katika runinga ya Tandao.
Ameongeza mtu yeyote anaweza kupata vipindi vya televisheni kwenye tovuti ya tandao na kuelezea kwa ufasaha jinsi mtu anaweza pata jukwaa hili katika simu yake.
Mtu yeyote anaweza kupata vipindi vyote vya Tandao tv kutoka jukwaa la golive afrika hasa mashabiki waaminifu wa runinga ya Tandao kutoka Nairobi, Kiambu miongoni mwa wengine ambao wamelalamika kuhusu masuala hiyo ya hali mbaya ya miw3; Tandao.
Mkurugenzi mkuu wa runinga ya tandao pia ameongeza kuwa mtu yeyote anaweza tazama vipindi vyote kwenye jukwaa hili kutumia hela kidogo.
Alitumia hotuba hiyo pia kuwathamini mashabiki wake waaminifu haswa kutoka mataifa mengine kama Ujerumani urusi Uholanzi na afrika kusini.
By Marion Halil