Madhara ya maradhi ya kichocho kuchukua mkondo tofauti

0
1

Wizara ya afya kwa ushirikiano na serikali za kaunti na shirika la afya ulimweguni WHO limeanzisha utafiti wa kubaini athari za kichocho katika ukanda wa Nyanza haswa kwa watoto wa shule waliokaribu na ziwa victoria.

Ugonjwa wa kichocho (Bilharzia) hupatikana katika nchi za tropiki na husababishwa na minyoo ya schistosoma ambayo huishi katika mito na maziwa ya maji. Takwimu ya wizara ya afya inaonyesha takriban watu million mia mbili na arobaini duniani wameambukizwa kichocho.

Wahudumu wa afya katika kaunti ya siaya wamehudhuria kongamano la siku moja ili kubadili namna ya kuwafikia walengwa wote katika wadi na kupokea mafunzo ya jinsi ya kubaini athari katika ukanda wa nyanza. Kulingana na Millicent Okwach ambaye ni afisa wa utafiti idara ya afya Siaya anaelezea kuwa wako na watafiti wengi katika viungo vya maji .

“Tuko na watafiti wengi kando ya vyazo vya maji huko rarieda na bondo na kupitia kwa utafiti huu unaopangwa na kwa kweli kuna masomo ya kuingilia kati ambayo hata huenda mbele na kuingilia kati,” alisema Millicent Okwach.

Katika kila wodi watafiti watatembelea shule tano ambazo zitachaguliwa kwa vigezo vya umbali wa viungo vya maji na shule na kuzingatia historia ya data inayoonyesha sehemu ambazo zimo katika hatari kubwa ya maambukizi. Aidha, lalama zimeelekezwa kwa serikali kwa kukosa kuwajibikia swala hilo la kukandamiza ugonjwa huo na hivi sasa wanadai kongamano hilo linalenga kutoa tiba.

“Haya ni magonjwa ya tropiki yaliyopuuzwa na utapata serikali ya kitaifa pamoja na ya kaunti hawajatenga rasilimali zozote ili kuyaondoa au kuyadhibiti lakini sasa hivi lengo letu ni kuyaondoa,” alisema mtafiti.

Ugojwa huu kwa muda mrefu umeweza kuwatatiza watu wengi ikiwema wahudumu wa afya kwani dalili zake zinafanana na ugonjwa kama vile kisonono na maradhi mengine. Hapa nchini ugonjwa huo unatibika kwani kuna dawa katika kila hospitali nchini.

Na Emmaculate Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here