Hamna ulaghai tena; serikali kusambaza mbolea moja kwa moja kwa wakulima

0
7

Naibu gavana kaunti wa Uasin Gishu John Barorot amesema serikali ya kaunti hiyo itasambaza mbolea moja kwa moja kwa wakulima, ili kuondoa dhiki ya ubroka kwa wakulima. Barorot aliyasema haya alipozuru kituo cha mafunzo ya kilimo cha Chebororwa kuhusu mbolea ya bei nafuu inayosambazwa na serikali.

Wizara ya kilimo ilitangaza bei mpya za mbolea baada ya wakulima kulalamikia bei za juu za mbolea. Serikali imewekeza shilingi billioni tatu nukta tano ili kuwapa afweni wakulima wanaohitaji mbolea kwa bei nafuu msimu wa upanzi.

Rais William Ruto aliagiza wizara husika kutoa mifuko millioni moja nukta nne ya mbolea kwa bei ya shillingi elfu tatu mia tano kwa kila mfuko wa kilo hamsini ulio kuwa shillingi elfu sita mia tano hapo awali.

Bei mpya ya mbolea ilianza kutekelezwa septemba tarehe kumi na tisa na kuanza kusambzwa katika maeneo yaliyokuwa yakipokea mvua chache. Hatari kwenye kilimo ilidhihirika baada ya  janga la korona na wakati huu wa vita kati ya Ukraine na Russia ambavyo vimepunguza idadi ya chakula na mbolea kutoka nje.

Kaunti mali mbali zinapanga kushiriki katika usambazaji wa moja kwa moja wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima msimu ujao wa upanzi.

Naibu gavana wa Uasin Gishu John Barorot alisema kuwa serikali ya kitaifa tayari imezitaka kaunti kujiandaa kusambaza mbolea hiyo kwa wakulima.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, naibu wa gavana John Barorot amesema serikali ya kaunti ya Uasin Gishu itawasambazia wakulima wa kaunti hiyo mbolea moja kwa moja ili kuwanusuru kutokana na madhara ya mabroka wenye tamaa.

Alisema watashirikiana kwa karibu na maafisa kutoka serikali ya kitaifa ili kuhakikisha mpango huo unafanya kazi kwa wakulima.

“Serikali ilituomba kujiandaa kuanza kusambaza mbolea ya ruzuku moja kwa moja kwa wakulima kuanzia msimu ujao,” Barorot alisema.

Alizungumza wakati wa mkutano wa wakulima katika chuo cha mafunzo kwa wakulima cha Chebororwa huko Uasin Gishu.

Hapo awali serikali imekuwa ikitumia NCPB kusambaza mbolea hiyo lakini shirika hilo hivi majuzi lilikabiliwa na mashambulizi makali kutokana na usambazaji wake duni wa mbolea ya ruzuku. Hii ilisababisha malalamiko makubwa  ya mara kwa mara kutoka kwa wakulima.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here