Serikali kuendeleza mfumo wa Ukulima wa GMO licha ya kupingwa vikali na wengi

0
0

Serikali kuu inayoongozwa na rais William Ruto inaendelea na mipango ya kupiga jeki swala la ukulima wa vyakula vya GMO hata baada ya maoni ya baadhi ya wakenya na viongozi kupinga ukulima wa vyakula hivyo. Serikali tayari imetenga ardhi ekari laki tano ili kupanda mahindi ya GMO huku ikilenga kuwapa wakulima mbegu ya GMO mwaka ujao.

Kilio cha baadhi ya wakenya kuhusiana na tishio la vyakula vya gmo kwa afya ya binadamu kinaonekana kusalia kilio tu kwani serikali kuu inayoongozwa na rais william ruto inaeendelea na mipango ya kupiga jeki swala la ukulima wa vyakula vya GMO.

Kulingana na daktari eluid kirega serikali tayari imetenga ardhi ekari laki tano ili kupanda mahindi ya GMO huku ikilenga kuwapa wakulima wa mbegu ya gmo mwaka ujao. Serikali inatazamia kutoa mbegu za mahindi zilizobadilishwa vinasaba (GMO) kwa wakulima mapema mwaka ujao.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la utafiti wa kilimo na mifugo nchini Dkt Eliud Kiplimo Kireger alisema tani 11 za mbegu za mahindi zilizoidhinishwa za GMO zitatolewa kwa wakulima wakati wa msimu wa mvua mrefu unaoanza machi na aprili.

“Mbegu hizo zitapandwa na wakulima kwenye ekari 500,000 katika maeneo ya mwinuko ya kilimo-ikolojia kama maandamano, kusubiri biashara kamili ya makampuni binafsi,” anasema.

Daktari James Karanja pia ameshikilia kuwa mipango hii inalenga kukabiliana na baa la njaa maeneo kadhaa nchini haswa wakati huu ambapo takriban wakenya milioni tatu wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Hata hivyo kenya ilikuwa nchi ya kwanza katika afrika mashariki kuidhinisha matumizi ya vyakula vilivyopigwa marufuku. Hii ni baada ya kuondolewa kwa marufuku hiyo ambayo imekuwepo kwa miaka kumi, ikumbukwe utumiaji na uingizaji wa vyakula vya GMO nchini ilikuwa haramu.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here