Zaidi ya watu milioni 4.2 wanaathirika na baa la njaa

0
1

Mikakati zaidi inazidikuzinduliwa ili kufanikisha  kusambaza vyakula vya msaada kwa familia zilizoathirika na ukame nchini. Kulingana na taarifa iliyotolewa na halamshauri ya kukabiliana na ukame NDMA mwanzo wa mwezi huu, zaidi ya watu milioni 4.2 wameathirika na wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.  

Hali ngumu ya maisha inaendelea kushuhudiwa na wananchi katika kaunti 29 nchini zinazokumbwa na ukame. Hali hii imewalazimu wakaazi kutegemea vyakula vya misaada kutoka kwa wahisani. Eneo la Loitoktok kaunti ya kajiado familia zaidi ya mianane  zimeathirika kwa miaka mitatu sasa hata bila dalili zozote za tone la mvua hali ambayo inazidi kuwahangaisha.  

“Hatujawahi pata chakula cha msaada na tunaomba serikali ya rais Ruto kwa kuwa bado hawajajipanga, wajipange na watuletee msaada wa chakula kabla hatujaangamia kwa njaa,“ mkaazi ; Kajiado
Wakaazi hawa wanadai kuwa licha ya kupokea vyakula vya misaada. bado havitoshi kuzikimu familia zao . hivyo wanaitaka serikali kusambaza vyakula vingi.  

Katika kaunti ya Garisa familia zaidi ya 10800 zimenufaika na usambazaji wa lishe ya mifugo. Hali ya ukosefu wa lishe ya mifugo iliwapelekea wakaazi kuhamia sehemu mbalimbali kuwalisha mifugo wao hali ambayo ilisababisha mizozo baina yao na wakaazi wa  sehemu wanakohamia.

 “Nataka kuwaambia wenye mifugo kuwa, hampaswi kuchunga mifugo wenu katika mashamba ya watu wengine. lazima tuje pamoja tuzungumze na kutatua shida zetu kwa pamoja.“ Mkaazi ; Garissa
Vile vile kaunti ya Machakos zaidi ya familia elf miamoja na harobaini na wanne katika maeneo tisa wamepata afueni kwa kupokea vyakula vya misaada. Huku usambazaji zaidi ukitarajiwa kufikia shule zote zilizo katika kaunti hii.

Gavana wa kaunti ya mMachakos Wavinya Ndeti ameagiza kujengwa kwa vidimbwi vya maji ili kusaidia wakaazi haswa wakati huu wa ukame.

“Leo tunapata chakula kwa familia zetu na pia shule zetu tumepeana mbegu watu waanze kyupanda vyakula. pia tumeagiza mbegu zaidi kutoka kwa serikali sasa naomba tusubiri zile tumeagiza huku tukipanga namna ya kutumia hizi tulizopokea,” Gavana; Machakos.

Serikali inazidikuombwa na familia zilizo maeneo kame ambazo zimeathirika na baa la njaa kuzidi kusambaza vyakula vya misaada.

Na Juliet Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here