Msichana mwenye miaka 17, Kirinyanga amuua babake sababu, chakula

0
5

Eneo la Ndindiriku Mwea kaunti ya Kirinyaga ni Kijiji kilicho wachwa kwa mshangao baada ya polisi kumtia nguvuni msichana wa miaka 17 kwa kudaiwa kumwua babake wa kambo wa miaka 34. Kulingana na polisi, mshukiwa alimdunga babake wa kambo kisu baada ya msichana huyo kukataa kumhudumia chakula cha jioni alichoitisha baada ya mamake kuenda mkutano wa kanisa.

“Msichana yule ambaye alikuwa amemdunga kisu ameshikwa na polisi na hiyo kisu ikachukuliwa kama ‘exhibit’ na msichana ako kituo cha polisi, mashtaka inafunguliwa na atapelekwa kortini baada ya uchunguzi.” Mkuu wa polisi kituo cha Mwea alisema.

Mamake anasema kwamba msichana huyo aliwahi jaribu kubakwa na babake wa kambo na huwa hawaongeleshani wakiwa nyumbani. Hii ni kwa sababu hawaelewani tangu msichana huyo akiwa darasa la saba ambapo babake wa kambo alijaribu kumbaka.

Haya yanajiri huku polisi katika kaunti ya Trans Nzoia wakianzisha msako wa kumsaka kijana wa umri wa miaka 21 Brian Wafula anayedaiwa kumuua mamake wa miaka 59 Judith Nafula na baadaye kutupa mwili wake katika mto wa Kiminini.

Mwendazake alikua mhudumu wa maabara katika shule ya upili ya wasichana ya St. Josephs Kiminini aliyeonekana mwisho tarehe kumi na nane mwezi huu baada ya kuzozana na mwanawe. Mwili wake baadaye ulipatikana ukielea majini.

“Alikuwa na maandalizi ya ‘practicals’, akaandaa maabara vizuri ila siku ya mtihani wa ‘practicals’ hakuonekana.” Mmoja wa wanaomjua alisema.

“Brian alikuwa mkali, akataka kumpiga mamake, na akatishia mamake maisha akasema kwamba ‘wewe ni kitu kidogo sana kwangu, naweza kukumaliza sai na hata simu ambayo umekamata kwa mkono hautakuwa na uwezo wa kuwaambia askari ama baba ama chief.” Mwingine aliongeza.

Kwingineko katika kaunti ya Nandi watu wawili wameuliwa baada ya kuvamiwa na mwanamume kwa tuhuma za kukuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. Inadaiwa kwamba Japheth Kimutai alishikwa na hasira na kuwaua.

Mkewe Japheth alikuwa anafanya kazi katika shamba la majani chai la mmoja wa waliouliwa. Kulingana na Japheth alivyodhania, ni kwamba mkewe alikuwa anahusiana nao kisiri na baadaye akagundua kabla ya kutekeleza Mauaji hayo.

Katika kaunti ya Kiambu, watu wanne wanauguza majeraha katika hospitali ya Gatundu Level 5 baada ya kushambuliwa kwa panga baada ya kile kinachochukuliwa kuwa kisa kinachohusisha mapenzi. Tukio hilo limewaacha wakazi wa kijiji cha Kiganjo ambapo shambulio hilo lilitokea kwa bumbuwazi kwanini mhusika angewashambulia hata wale waliofika kuwaokoa waliokuwa wakishambuliwa.

Na Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here