Kenya yapiga hatua kubwa katika kukuza misitu

0
16

Licha ya serikali ya kitaifa kufanya bidii na kufikisha asilimia 12.5 ya misitu mwaka huu kaunti ya Busia imetajwa kuwa na kiwango cha chini mno cha misitu huku wakishika dau wakiendeleza juhudi za kuongeza idadi hiyo.

Afisa anayesimamia idara ya kutunza misitu katika kaunti ya Busia Vitalis Osodo ameeleezea kufurahia kuwa licha ya Kenya kutakiwa kufikisha asilimia 10 ya misitu kufikia mwaka wa 2022, imepitisha idadi hiyo hadi asilimia 12.5.

Akizungumza katika chuo kikuu cha Alupe eneo bunge la Teso Kusini kaunti ya Busia wakati wa hafla ya kusherehekea kuzaliwa kwa mmoja wa mashujaa waliopigania uhuru Dedan Kimathi, Osodo amefichua kuwa kaunti ya Busia imefikia asilimia 3.5 pekee ya malengo hayo na sasa wanashirikiana na washikadau kupanda miti kwa wingi.

“Katika kaunti ya busia bado hatujaafikia matarajio yetu katika upanzi wa miti. Na njia mojawapo ya kubambana na ukame ni kwa kupanda miti kwa wingi,” Vitalis Osodo ; msimamizi wa idara ya kutunza misitu Busia.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, msimamizi wa wakfu wa Dedan Kimathi, Mickson Maina amesema kuwa wameanzisha mpango wa upanzi wa miti kote nchini ili kuongeza idadi ya miti na misitu kama mojawapo wa njia za kuwatuza mashujaa waliopigania nchi hii.

 “Tuko hapa kwa ajili ya kusherehekea miaka mia moja ishirini na mbili ya akuzaliwa kwa Dedan Kimathi aliyeongoza katika kupigania haki za kibinadamu kwa kutumia msururu wa mau mau. Kupanda miti ni njia mojawapo ya kuyahenzi mazingira ambayo yalitumika kama sehemu za kujificha wakati wa vita vya kikoloni,” Dickson Maina msimamizi wa wakfu wa Dedan Kimathi.

Hata hivyo mwanamazingira katika kaunti ya Busia kutoka kwa shirika la linda mazingira Patrick Ikwara amesema kuwa licha ya washikadau kufanya bidii na kupanda miti kwa wingi ni vyema miti hiyo kutunzwa ipasavyo ili kuafikia malengo ya serikali.  

“Kwa mfano katika kaunti ya Busia tukipanda miti itanawiri vizuri. Hata hapa alupe tumejaribu mara mingi sana kupanda miti lakini kwa sababu ya mlipuko wa ebola katika nchi jirani  ya Uganda utapata kuwa waganda wanaingia humu nchini kulisha mifugo wao na pia kuiba miti,“ Patrick Ikwara mkurugenzi wa Linda Mazingira.

Wakati huo huo mmoja wa wasimamizi katika chuo kikuu cha Alupe Profesa Emmy Kipsoi amesema kuwa wamelenga kuhakikisha kuwa zaidi ya miti milioni moja inapandwa katika chuo hicho kama juhudi za kutunza mazingira ya taasisi hiyo. 

By Juliet Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here