
Kulingana na hotuba ya Rais William Ruto katika maadhimisho ya siku kuu ya Mashujaa,alisema kwamba nchi hii inalenga kukuza miti bilioni kumi na tano ifikapo mwaka wa elfu mbili
thelathini na mbili (2032). Hii ni njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga
ambayo imesababisha ukame kukithiri katika kaunti mbalimbali nchini.
“This will eventually lead to the rehabilitation and restoration of 10 million hectares in our 290
constituencies and some special selected ecosystem and water towers threatened by degradation
and destruction.” The President said.
Ili kufanikisha upandaji wa miti bilioni kumi na tano, itambidi kila mkenya kupanda na kukuza
miti mia tatu na kulingana na Rais, atakayekamilisha atapata cheti kutoka kwa wizara ya
mazingira.
“I will tell the ministry concerned, the Ministry of environment to issue a small certificate for
every Kenyan who completes his/her round of 300 trees.” The President.
Rais Ruto anapania kuongeza kiwango cha misitu na miti nchini hadi asilimia thelathini ifikiapo 2032. Mpango huu amesema unaweza kufanikishwa iwapo wakenya watahusika kwa kupanda
miti.
Kulingana na rais, kaunti zilizo na asilimia ya juu ya misitu ni;
Nyeri
Lamu
Vihiga
Kirinyaga
Elgeyo-Marakwet
Meru
Embu
Murang’a
Kilifi
Nyandarua
Zilizo na asilimia ya chini ni;
Marsabit
Mandera
Wajir
Isiolo
Siaya
Migori
Busia
Machakos
Taita Taveta
Uasin Gishu
Rais pia aliamuru kuteuliwa kwa makurutu 2700 na maafisa mia sita watakaojiunga na idara ya
misitu KFS ili kuboresha ulinzi wa misitu.
Nchi hii imekumbwa na ukame katika sehemu mbalimbali nchini na wafugaji wameumizwa
sana. Pia wanyamapori wameathirika pakubwa. Iwapo mpango wa Rais utatiliwa manani, hali
inaweza kubadilika.
Waziri mteule wa mazingira Soipan Tuya katika mahojiano ya kupigwa msasa pia alisisitiza
suala la msitu. Alisema kwamba iwapo atapewa nafasi, hatua yake ya kwanza itakuwa kuokoa
mnara wa maji, msitu wa Mau. Alisema ataanzisha awamu ya pili ya kuweka ua.
“I have looked at the budgetary, the pending budget for the completion of the fencing of the
Mau. The President is also very clear that it is a question of immediate action that we are going
to take to complete the fencing of the Mau.” Soipan Tuya.
Suala la Mau limekuwa suala nyeti kwa muda mrefu. Mwaka wa 2019, serikali ilitoa Hekta elfu
arubaini na nne za msitu wa Mau zilizokuwa chini ya walowezi eneo la Mau Narok. Shughuli za
kuweka ua eneo hilo imekuwa ikiendelea
Pia alisisitiza suala la uchafuzi wa mito, suala ambalo pia ni tata. Alisema atahakikisha
ameangazia suala hilo kwa kina sana. Changamoto ya kushughulikia uchafuzi wa mito na
ukosefu wa miundo misingi ni kero atakayolazimika kushughulikia.
Suala la mabadiliko ya hali ya anga likitiliwa mkazo na serikali ya Rais William Ruto, basi
wakenya wataweza kupata afueni katika sekta ya njaa na ukame.
Na Calvin Angatia