Naibu wa Rais Gachagua azindua shehena ya pili ya mbolea

0
5

Huku baa la njaa likiathiriwa kaunti zaidi ya ishirini na tisa serikali ya kenya kwanza imejizatiti hii ni kufuatia uzinduzi wa shehena ya pili ya mbolea na naibu rais Rigathi Gachagua ambayo inanuwia kuboresha kilimo haswa cha majani chai. Katika hafla ya kusherekea siku ya mashujaa nchini rais William Ruto aliyoa ahadi kwa sekta ya kilimo kwamba serikali yake itawasilisha mbolea nyingine kabla ya msimu wa mvua unaoanza machi hadi Julai ilikuboresha kilimo nchini.

Naibu wa rais amezindua shehena ya pili ya mbolea ya bei nafuu ambayo ni afueni kwa wakulima huku ikinuwiwa kuboresha kilimo nchini kwani kilimo ni uti wa mgogo wa nchi hii.

“Kutiwa alama kwa shehena hii ya pili ya mbolea kwa wakulima wa chai kote nchini kutapunguza mzigo wa wakulima kwa njia kubwa kwani mbolea iliyokuwa ikiuzwa kwa shilingi elfu sita sasa itauzwa kwa shilingi elfu tatu mia tano,”alisema Gachagua bei ya mbolea hiyo imepunguzwa kutoka shilingi elfu sita hadi elfu tatu na mia tano na inatarajiwa kupungua zaidi hii ni baada ya serikali ya Kenya Kwanza kuahidi kupungua kwa bei.

Gachagua ameelezea kuwa wananuia kufadhili sekta ya kilimo nchini ilikuimarisha mazao ambalo litawezesha mauzo ya nje haswa majani chai.

“Nataka niwaombe wakulima wetu kote nchini mara tu watakapopata mbolea hii waitumie ipasavyo, watunze majani chai yao na kuhakikisha tunapata chai bora” alisema Gachagua.

Kenya ni nchi ya tatu ulimwenguni baada ya nchi ya uchina na india kwa uzalishaji na uzaji wa majani chai katika maoko za kimataifa katika nchi za kigeni. Vilevile ameahidi kuimarisha kilimo cha majani chai na kuwarai wakulima kukumbatia ukuzaji kwani soko la kimataifa liko imara katika nchi za kigeni.

Na Emmaculate Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here