Zoezi la mchujo wa mawaziri teule kutamatika: Je, umeridhika?

0
3

Bunge la kitaifa lilitoa ratiba ya kuwachuja mawaziri walioteuliwa  katika baraza la mawaziri na rais William Ruto. Hafla hii ilichukuwa takriban wiki moja.

Katika taarifa iliyotolewa na karani wa bunge la kitaifa Sarah Kioko , mawaziri wote walioteuliwa walitengewa muda na siku mahususi watakapofika mbele ya kamati ya uteuzi

Wagombea hao walitakiwa kuwasilisha mbele ya kamati vitambulisho vyao halisi, vyeti vya taaluma na barua za kibali na kufuata sheria kutoka kwa EACC, KRA, HELB, DCI na CRB

Shughuli ya mchujo ilifanywa na kamati ya watu kumi na watano walioongozwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula.

 Kulingana na ratiba ya karani wa bunge Serah Kioko, katibu mkuu mteule wa baraza la mawaziri Musalia Mudavadi ndiye alikuwa wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo kuhusu uteuzi saa tatu asubuhi akifuatwa na Justin Muturi  saa 10.30 nne unusu.

Waliokaguliwa pia  siku ya kwanza ni Aden Duale waziri mteule wa ulinzi,  Alfred Mutua waziri mteule wa masuala ya kigeni na diaspora na alice muthoni wahome waziri mteule wa maji na usafi wa mazingira.

Siku ya pili, jumanne, oktoba 18, 2022, kamati ilichunguza Kithure Kindiki (utawala wa ndani na kitaifa Njuguna Ndung’u (hazina ya kitaifa na mipango), Aisha Jumwa (utumishi wa umma, jinsia na hatua ya uthibitisho), Davis Chirchir (nishati na petroli) na Moses Kuria (biashara, uwekezaji na viwanda).

Siku ya tatu, jumatano, 19 oktoba 2022, kamati ilitahakiki:o Onesmus Kipchumba Murkomen (barabara, uchukuzi na kazi za umma)Rosalinda Soipan Tuya (mazingira na misitu)Peninah Malonza (utalii, wanyamapori na urithi)Zacharia Mwangi Njeru (ardhi, nyumba na maendeleo ya miji)susan nakhumicha wafula (afya).

Siku ya nne, ijumaa tarehe 21 oktoba 2022, waliochunguzwa ni mithika linturi (kilimo na maendeleo ya mifugo)Eliud Owalo (mawasiliano ya habari na uchumi wa dijitali)ezekiel machogu (elimu)Ababu Namwamba (masuala ya vijana, michezo na sanaa)Rebecca Miano (jumuiya ya afrika masharikiardhi kame na nusu kame na maendeleo ya kikanda).

Siku ya tano na ya mwisho, jumamosi tarehe 22 oktoba 2022, mawaziri waliochujwa ni simon chelugui (ushirika na maendeleo ya biashara ndogo, ndogo na za kati) Salim Mvurya (madini,uchumi wa bluu na mambo ya bahari)Florence Bore (ulinzi wa kazi na jamii)Mercy Wanjau (katibu wa baraza la mawaziri).

Na Marion Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here