Kufungwa kwa Waluke kwazua balaa

0
5

Shughuli muhimu zikiwemo usafiri na biashara katika eneo bunge la sirisha kaunti ya Bungoma zililemazwa kufutia maandamano yaliyotokana na kushikwa na kutiwa gerezani kwa mbunge wa eneo hilo john waluke. Wakaazi hawa wanadai kuwa kushikwa kwa mbunge huyo kunazidi kulemaza utendakazi wa eneo bunge hilo na hivyo wanamtaka rais william ruto amuachilie.

Shughuli mingi za wakaazi na wafanyibiashara eneo bunge la sirisha kaunti ya bungoma zililemazwa huku wakazi wa eneo hilo wakiandamana kufuatia kushikwa na kufungwa kwa mbunge wao John Waluke.

Wakaazi hawa wenye ghadhabu walisema kuwa waluke hana hatia na amechangia pakubwa kuwepo kwa chama cha UDA katika kaunti ya bungoma. Aidha wakaazi hawa walionyesha kukerwa na hatua ya mbunge wao kutiwa kizuizini .na hivyo wanamtaka rais william ruto kuingilia kati ili kumuachilia huru mbunge huyu.

“Zile kura ambazo rais William Ruto amepata Bungoma ilikuwa kupitia kwa mbunge Waluke kumpigioa debe. Na mweshimiwa Waluke ndiye mwanzilishi wa UDA Bungoma. ndiye alimleta rais Wiliiam Ruto Bungoma Nna baadaye mweshimiwa amesingiziwa kesi na kutiwa gerezani, kwa hiyo tunamuomba bwana Rais amsaidie Waluke aachiliwe huru,“ Mkaazi wa sirisha; bungoma.

Mapema mwaka wa 2020 mahakama ilimpata mbunge huyo na hatia ya ulaghai katika bodi ya NCPP ambapo anashukiwa kufuja shilingi milioni 297. Wiki mbili zilizopita, mbunge huyo ghafla aliingiwa na wasiwasi baada ya mahakama ya juu kumtoza faini ya sh. 1B au kuhudumia mahakama kwa miaka 67 gerezani.  

Hatua hii haijawafurahisha wakaazi wa sirisha kwani wanamtaka waluke aachiliwe huru. pia wanamtaka aachiliwa ili apate kufuatilia kesi yake mahakamani.

“ Tunaomba aachiliwe huru ili aweze kufuatilia kesi yake katika koti ya rufaa na apate haki yake. mweshimiwa Waluke sio mwizi. Yeye ni mfanyibiashara na kwa hivo anazingiziwa wizi.“ 

Na Juliet Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here